Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Kiwanda cha dawa Keko, Shirika la Posta, Bodi ya Chai wapata hati mbaya, zenye shaka’

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wa Tanzania, Charles Kichere

Muktasari:

  • Kwa mwaka wa fedha 2023/24 CAG alifanya jumla ya ukaguzi idadi yake ikiwa ni 1,485, ukaguzi 1,301 zikiwa za hesabu za fedha, ukaguzi 15 wenye ufanisi na ukaguzi maalumu 52.

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wa Tanzania, Charles Kichere ameyataja mashirika manne ya umma yaliyopata hati zenye shaka na hati mbaya katika ripoti yake ya mwaka wa fedha 2023/24.

Miongoni mwa mashirika hayo ni pamoja na kiwanda cha dawa cha Keko Pharmacetical kinachozalisha dawa na vifaatiba mbalimbali ikiwemo barakoa.

CAG ameyasema hayo leo Alhamisi, Machi 27, 2025 alipokuwa akiwasilisha ripoti yake ya ukaguzi kwa Rais Samia Suluhu Hassan ya mwaka wa fedha 2023/2024 Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Taasisi zilizopata hati zenye shaka na hati mbaya ni pamoja na Kiwanda cha Dawa Keko, Bodi ya Chai Tanzania, Chuo cha Sukari cha Taifa na Shirika la Posta Tanzania haya ni mashirika ya umma,” amesema Kichere.

Katika upande wa miradi ya maendeleo, ameitaja Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru, Mfuko wa Afya pia zilipata hati mbaya.