Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kijana aliyepigwa risasi na polisi kuzikwa Jumatano

Muktasari:

  • Kijana Ng’ondi Marwa (22) aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi na askari polisi Machi 31 katika kijiji cha Kubiterere wilayani Tarime, anatarajiwa kuzikwa Jumatano hii.

Tarime. Familia ya Ng’ondi Marwa (22) aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi na askari polisi inatarajia kufanya mazishi ya kijana huyo Jumatano hii.

Mazishi hayo yanafanyika baada ya mazungumzo baina ya familia na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya baada ya awali familia kusema haitazika kutokana na kutokuwa na uwezo.

Akizungumza na Mwananchi jana baba wa marehemu, Marwa Masiaga alisema baada ya uchunguzi wa mwili wa marehemu, jeshi la polisi liliahidi kukutana nao kwa ajili ya taratibu nyingine.

“Leo asubuhi tumeenda pale kanda maalumu na tumekubaliana kufanya mazishi Jumatano ijayo, polisi wamesema watachangia sehemu ya gharama za msiba na sehemu nyingine tutagharamika sisi,” alisema.

Ng’ondi alifariki dunia Machi 31, katika Hospitali ya mji wa Tarime alilopelekwa kwa matibabu kutokana na majeraha ya risasi.

Inadaiwa siku hiyo asubuhi kijana huyo alikuwa na mifuko mitano ya saruji aliyonunua nchini Kenya na alipigwa risasi na askari polisi PC 4489 Kaluletela katika kijiji cha Kubiterere wilayani Tarime. Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya linamshikilia askari huyo huku likisema tukio hilo limefanywa na askari huyo binafsi si jeshi hilo.


Suhuda aeleza

Shuhuda Paulo Chacha alisema kabla ya kupigwa risasi askari aliyekuwepo eneo hilo alimtaka Ng’ondi kumpa Sh300,000 ili amruhusu kupita na mzigo.

“Alimwambia asipotoa kiasi hicho cha pesa angewataarifu watu wa TRA, jamaa akambembeleza lakini askari alikataa akawa anasema bila hiyo hela hapiti,” alisema. Alieleza askari alipokataa Ng’ondi aliamua kufungua mifuko aliyokuwa amepakia kwenye pikipiki kwa lengo la kuiacha pale ili aondoke na pikipiki, lakini askari huyo alimzuia kuondoka.

“Wakaanza kuvutana, nikaona askari anakoki bunduki mwanzoni nilijua anamtisha tu ndugu yetu baada ya muda akafyatua risasi mbili na Ng’ondi akaanguka chini wakati huo kuna askari mwingine anaangalia” alisema.