Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zelensky amfuta kazi kiongozi wa jeshi, shambulizi latajwa kuwa chanzo

Muktasari:

  • Vladimir Artyukh amemfuta kazi kufuatia madai kuwa alipanga hafla ya utoaji tuzo za kijeshi ambayo ililengwa katika shambulio la makombora ya Urusi katika Mkoa wa Sumy nchini humo lililosababisha vifo vya raia zaidi ya 35 na wanajeshi zaidi ya 60.

Kiev. Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amemfukuza kazi Mkuu wa Utawala wa Kijeshi katika Mkoa wa Sumy nchini humo, Vladimir Artyukh.

Vladimir Artyukh amefukuzwa kazi kutokana na madai kuwa alipanga hafla ya utoaji tuzo za kijeshi ambayo ililengwa katika shambulio la makombora ya Urusi katika Mkoa wa Sumy nchini humo lililosababisha vifo vya raia zaidi ya 35 na wanajeshi 60.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilithibitisha kufanya shambulio hilo lililolenga mkusanyiko wa maofisa wakuu wa Ukraine katika mji huo uliopo mpakani.

Urusi ilisema kuwa makombora mawili ya Iskander-M yalitumiwa katika shambulio hilo siku ya Jumapili  na kueleza kuwa wanajeshi 60 wa ngazi za juu wa Ukraine waliuawa.

Mamlaka za ndani za Ukraine zilidai kuwa shambulio hilo lililenga hafla ya utoaji tuzo za kijeshi kwa Brigedi ya 117 ya Ulinzi wa Taifa. Maofisa waliripoti kuwa shambulio hilo  liliwajeruhi watu 129.

Maofisa  kadhaa wa Ukraine, akiwemo Meya wa Konotop, Artyom Semenikhin, tangu kutokea shambulizi hilo, wametoa wito wa Artyukh kushtakiwa, wakimtuhumu kuhusika katika vifo hivyo kwa kupanga hafla ya tuzo licha ya onyo la kutofanya hivyo.

Artyukh amekiri kuwa hafla hiyo ilifanyika siku ya shambulio lakini alikana kuhusika moja kwa moja, akiiambia televisheni ya umma ya Suspilne kwamba alialikwa lakini hakuwa mpangaji wa tukio hilo.

Hata hivyo, Zelensky alisaini amri jana Jumanne ya kumuondoa Artyukh madarakani. Taras Melnychuk, ambaye ni Mwakilishi wa Baraza la Mawaziri bungeni, alithibitisha taarifa hiyo kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa Telegram na kutangaza kuwa Serikali imeshatea mrithi wake.

Hata hivyo, Urusi imesisitiza kuwa haiwalengi raia wala miundombinu ya kiraia nchini Ukraine. Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amesema jeshi la Urusi linashambulia popote penye malengo yanayohusiana na kijeshi.


Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa mashirika ya habari.