Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkuu Italia amtembelea Papa Francis hospitali, adokeza afya yake

Muktasari:

  • Papa Francis ambaye ni raia wa Argentina, yuko katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya mapafu kwa sababu alipokuwa kijana, alipata changamoto kwenye pafu lake moja iliyosababisha sehemu ya pafu hilo kuondolewa.

Sicily. Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, amesema hali ya kiafya ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis inatia matumaini.

Meloni ambaye alimtembelea Papa Francis jana katika hospitali alipolazwa akiugua nimonia ya mapafu, ameandika usiku wa kuamkia leo Alhamisi Februari 20, 2025, kwenye akaunti yake ya X (zamani Twitter) kuwa alimkuta Papa Francis akiwa mwenye kutia matumaini na akidokeza kuwa alizungumza naye huku akimtania.

Kwa mujibu wa taarifa ya Vatican, vipimo vya damu vya, Papa Francis vimeonyesha afya yake kuimarika kidogo, pia akiendelea kupata matibabu ya nimonia inayoelezwa ndio chanzo cha kuugua na kupelekwa hospitali.

Papa huyo (88) afya yake inatia matumaini huku madaktari wakiendelea kushughulikia tatizo lililobainika la maambukizi ya mfumo wa upumuaji.

Papa Francis alilazwa katika Hospitali ya Gemelli huko Roma, Italia, Februari 14.

“Hali ya kiafya ya Baba Mtakatifu iko thabiti, vipimo vya damu … Vinaonyesha anaimarika kidogo kidogo, hasa katika vichochezi vya mwili,” imesema taarifa fupi ya Vatican.

Awali, Vatican ilisema Papa alikuwa na maambukizi ya aina mbalimbali ya bakteria, ikiongeza kuwa angeendelea kubaki hospitalini atakaohitajika ili kushughulikia tatizo lake.

Ingawa Meloni na Papa Francis hawakubaliani kuhusu masuala ya wahamiaji, lakini amekuwa kiongozi wa kwanza kumtembelea kiongozi huyo wa kiroho hospitalini.

Ofisa mmoja wa Vatican ambaye jina lake halikuwekwa wazi, amesema mapema Jumatano kuwa Papa Francis hakuwa kwenye mashine ya kusaidia kupumua (Ventilator), bali alikuwa akipumua kwa uwezo wake mwenyewe.

Ofisa huyo alisema Papa, jana aliweza hata kutoka kitandani na kukaa kwenye kiti ndani ya chumba chake hospitalini, na alikuwa akiendelea kufanya shughuli ndogo ndogo.

Mahujaji waliokusanyika Vatican Jumatano kwa ajili ya mkutano wa kila wiki wa Papa uliokuwa umesitishwa nao walieleza matumaini yao juu ya kupata nafuu kwake.

“Tutamwombea apone haraka iwezekanavyo,” amesema Gianfranco Rizzo, Kiongozi wa kiroho kutoka Bari, Italia.

Victoria Darmody, ambaye ni mtalii kutoka Uingereza, amesema aliwasili katika Hospitali ya Gemelli ili kuwa karibu na Papa.

 “Tulitaka kuhudhuria mkutano wa Papa leo lakini tukahisi kuwa hapa ndiko mahali sahihi pa kuwa badala yake,” amesema Darmondy.

Papa huyo wa Argentina yuko katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya mapafu kwa sababu alipokuwa kijana, alipata changamoto kwenye pafu lake moja iliyosababisha sehemu ya pafu hilo kuondolewa.


Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa Mashirika.