Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri matatani kwa kuwaita waandishi wa NMG ‘Makahaba’

Waziri wa Biashara wa nchini Kenya, Moses Kuria

Kenya. Muungano wa Wanahabari wa Kenya (KUJ) pamoja na Kamati ya kuwalinda wanahabari barani Afrika (CPJ) imemjia juu Waziri wa Biashara wa nchini Kenya, Moses Kuria baada ya kutishia na kutoa matamshi tata kwa waandishi wa habari wa kampuni ya Nation Media Group(NMG) akiwaita ‘makahaba’.

Sakata la kuwashambuliwa wanahabari hao liliibuka siku chache baada ya Televisheni ya NTV inayomilikiwa na kampuni ya NMG kutoa taarifa ya uchunguzi inayoonyesha kashfa ya mpango wa uagizaji mafuta ya kupikia bila ushuru unaoendeshwa na shirika la serikali.

Kuria alitoa kauli hiyo isiyo ya kiungwana baada ya maofisa wa Serikali hiyo kuendelea kushirikiana na NMG katika matangazo ya vyombo vya habari huku akiwatishia kuwafukuza kazi endapo wakiendelea.

Aidha, waziri huyo alihoji kama chombo hicho cha habari kipo kwa ajili ya kutoa taarifa au chama cha upinzani. Siku inayofuatia Juni 18, Kuria alienda mbali zaidi na kuwatishia maofisa hao kuwafuta kazi serikalini.

Katika mfululizo wa tweets kati ya Juni 18 na Juni 20, Kuria aliwaita wafanyakazi wa kampuni hiyo ‘makahaba,’ akiwashutumu kwa rushwa na upendeleo, na kuahidi kuchapisha majina ya waandishi ambao wamekiri kulazimishwa kuandika kinyume habari za serikali.

Nayo kampuni ya NMG imesema kauli ya waziri huyo haina afya na nia njema katika uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.

"Shambulio la maneno lisilo na msingi la Kuria, si tu kwamba halikuwa na heshima kwa serikali, lakini ni shambulio dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari na msingi wa demokrasia," Daily Nation ilisema katika tahariri iliyochapishwa kwenye tovuti yake juzi Jumanne.

Katika taarifa yake aliyoitoa jana Jumatano Kuria amesema kuwa hataomba msamaha kutokana na kauli zake.