Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rajoelina ashinda urais Madagascar

Muktasari:

  • Rais Rajoelina ameshinda kwa asilimia 59 ya kura na hivyo kuwapiga chini wapinzani wake wawili wa karibu, ambao ni marais wa zamani wa nchi hiyo, Marc Ravalomanana na Siteny Randrianasoloniaiko.

Madagascar. Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina ameshinda muhula wa pili kufuatia uchaguzi unaodaiwa kuwa na utata kiasi cha kusababisha upinzani nchini humo kuhamasisha wafuasi wao kuususia.

 Inaelezwa  kuwa rais Rajoelina ameshinda kwa asilimia 59 ya kura na hivyo kuwapiga chini wapinzani wake wawili wa karibu, ambao ni maraisi wa zamani wa nchi hiyo, Marc Ravalomanana na Siteny Randrianasoloniaiko.

BBC imeripoti kuwa katika uchaguzi huo, idadi ndogo ya wapiga kura wanadaiwa kujitokeza ikiwa   ni chini ya asilimia 46 ya watu waliokuwa wamejiandikisha kupiga kura.

Inaelezwa uchaguzi huo kuwa na wapiga kura wachache katika historia ya nchi hiyo.

Dulu za siasa zinadai kuwa idadi hiyo ndogo ya waliojitokeza kupiga kura, inafuatia wito wa kususia uchaguzi huo iliyotolewa na wagombea 10 wa urais, kutoka vyama vya upinzani.

Wagombea hao walijiondoa katika kinyang’anyiro hicho baada ya kuonyesha wasiwasi wao juu uchaguzi huo  wakituhumu uwepo wa dalili za haki kutotendeka, huku wakihoji uhalali wa rais Rajoelina kuwania kiti hicho kutokana na kudaiwa kuwa na uraia wa nchi mbili ikiwemo Ufaransa.

Hata hivyo, Mahakama ya kikatiba nchini humo, ilitupilia mbali shutuma hizo zikionekana  ni mbinu za kisiasa.

Licha ya kujitoa kwa wagombea hao 10 kutoka upinzani, majina ya wagombea bado yalibaki katika karatasi za kupigia kura, na hivyo kuonyesha Randrianasoloniaiko akiwa amepata asilimia 14 ya kura zilizopigwa, huku Ravalomanana akipata asilimia 12 ya kura zote.

Mahakama ya kikatiba ina siku tisa kuthibitisha matokeo yaliyotangazwa leo Jumamosi na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo (Ceni).

Muungano wa upinzani ambao ulisusia uchaguzi tayari umetangaza kuwa hautatambua matokeo ya uchaguzi huo wa Novemba 16.

Kabla ya uchaguzi huo, kambi ya upinzani nchini humo iliitisha maandamano kwa muda wa wiki sita, ambayo yaligubikwa na mapigano na polisi, jambo lililosababisha kutangazwa kwa amri ya kutotoka nje usiku mmoja kabla ya uchaguzi katika jijini Antananarivo.

Rajoelina (49), ni mfanyabiashara na amewahi kuwa DJ, aliingia madarakani mwaka 2009 baada ya mapinduzi ya kijeshi, hata hivyo hakugombea uchaguzi uliofuata.

Mwaka 2018, Rajoelina alishinda kura ya marudio ya uchaguzi wa rais dhidi ya Ravalomanana baada ya wagombea wote kukosa asilimia 50 ya kura zinazotakiwa kikatiba.

Mwanasiasa huyo anakabiliwa na kibarua kigumu cha kutengeneza ajira na kuboresha uchumi, katika nchi ambayo kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia (WB), asilimia 75 ya watu wake ni masikini.

Pia anatakiwa kuhakikisha kunakuwa na utulivu wa kisiasa katika nchi hiyo iliyogubikwa na misukosuko ya kisiasa kwa miaka mingi.