Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Ruto awajibu Wakenya kutumia gharama kubwa safari ya Marekani

Muktasari:

  • Rais wa Kenya, William Ruto amekanusha madai ya kutumia gharama kubwa ziara yake ya simu nne ya Marekani.

Dar es Salaam. Rais wa Kenya, William Ruto amejibu madai ya kutumia gharama kubwa kwenye ziara yake ya Marekani kwa kukodi ndege binafsi.

Hatua ya Rais Ruto kujibu madai hayo kwa kukanusha inakuja wakati minong’ono ikisambaa ndani na nje ya Taifa hilo kuwa alitumia zaidi ya Sh4 bilioni.

Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) amekanusha madai hayo kwa kusema wala haikuwa gharama kubwa kutumia ndege hiyo.

Rais Ruto ameandika hayo leo Jumapili Mei 26, 2024 huku akidai gharama ingekuwa kubwa zaidi kama angetumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ).

“Wakenya wenzangu, nimeona wasiwasi wenu kuhusu njia yangu ya usafiri hadi Marekani. Kama msimamizi anayewajibika wa rasilimali za umma na kulingana na azimio langu la kuishi kulingana na uwezo wetu, napaswa kuongoza kwa kuwa mstari wa mbele, gharama ilikuwa ndogo kuliko kusafiri kwa KQ.”

Mei 19, 2024 Rais Ruto alifanya ziara ya siku nne nchini Marekani na alikaribishwa na mwenyeji wake Rais Joe Biden huku yakiibuka maneno hususani katika mitandao ya kijamii.

Awali, ilielezwa kuwa safari ya ndege ya kwenda njia moja kutoka Nairobi hadi Atlanta, kama ilivyonukuliwa na Royal Jet, ni sawa na Dola 748,600 (Sh1.94 bilioni) kwa safari ya saa 18.

Safari ya Rais Ruto kwenda na kurudi Washington (saa mbili), gharama ya jumla inaweza kuzidi Sh4 bilioni.

Pia, kupitia habari iliyochapishwa na The Standard na KTN News, matumizi hayo yatawagharimu walipakodi.

Awali, Gazeti la The Standard liliripoti kwamba walipa kodi watalipa gharama kubwa kwa safari ya Ruto. Ikulu imekodi ndege ya biashara ya Boeing 737-700 inayoendeshwa na Kampuni ya Royal Jet ya Dubai.

Ndege hiyo ya kifahari inahudumia soko kati ya UAE, Ulaya na Marekani. Gharama ya kukodi ndege hii ni Dola 18,000 za Marekani (Sh46.7 milioni) kwa saa.

Hata hivyo, kutokana na sakata hilo, Serikali ya Marekani ilifafanua haijaidhinisha malipo ya ndege binafsi ya Rais Ruto kwenda Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jumanne, Mei 21, 2024, Msemaji wa Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi, Andrew Veveiros alisema: "Kwa kweli, Marekani haikulipia ndege ya Rais Ruto kwenda Marekani."