Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi watano wauawa kwa kupigwa risasi

Muktasari:

  • Polisi watano wameuawa nchini Nigeria kufuatia shambulizi la risasi lililofanywa na watu waliojihami na silaha Kusini Mashariki mwa Jimbo la Imo.

Nigeria. Watu wenye silaha wamewaua maofisa watano wa polisi wa Nigeria na raia wawili wakati wa shambulio kusini mashariki mwa Jimbo la Imo jana Ijumaa.

Makundi yenye silaha yameshambulia vituo vya polisi na ofisi za serikali na uchaguzi katika majimbo ya kusini mashariki, ambapo serikali imelaumu kundi lililopigwa marufuku la watu wa asili ya Biafra (IPOB) japo watu hao wamekanusha kuhusika.

Msemaji wa polisi wa Jimbo la Imo, Henry Okoye amethibitisha kifo cha maofisa hao na raia lakini hakutoa maelezo zaidi.

Nigeria inakabiliwa na ukosefu wa usalama ulioenea, huku mashambulizi ya bunduki na utekaji nyara kaskazini-magharibi, kukithiri kwa waasi wa kidini kaskazini mashariki na vurugu za kujitenga na magenge kusini mashariki mwa nchi.

Tukio hilo ni mwendelezo wa majaribio ya kutaka kujitenga kwa eneo lilipo Kusini Mashariki liliko Kabila la Igbo.

Eneo hilo lilijaribu kujitenga mwaka wa 1967 chini ya jina la Jamhuri ya Biafra na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitatu ambapo zaidi ya watu milioni moja walikufa, wengi wao wakifa kwa njaa.