Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwandishi wa habari akutwa amejinyonga nyumbani kwake

Kenya. Mtangazaji wa zamani katika kituo cha Redio cha Pwani FM, Sammy Ambari (48), amekutwa nyumbani kwake akiwa amefariki dunia kwa kujinyonga.

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Mkongani, eneo la Matsangoni, Kaunti ya Kilifi nchini Kenya, juzi na kutolewa taarifa leo Jumanne Septemba 26, 2023 kupitia mitandao ya kijamii ya kituo hicho cha redio.

Sammy ambaye enzi za uhai wake alifahamika kwa jina la utani ‘Mtumishi’ alipata kupitia kipindi cha ‘Tumsifu Bwana’ kilichorushwa kila Jumapili kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu asubuhi.

Mdogo wa marehemu, Morris Ambari amethibitisha kutokea tukio hilo siku ya Jumapili.

“Nilimuita ndugu yangu kwa ajili ya kunywa chai asubuhi Jumapili lakini alikataa na baadaye tulimkuta akiwa amejitundika kitanzi,” amesema Morris.

Amesema alimkuta akiwa amejinyonga kwenye chumba cha watoto kilichopo ghorofani katika nyumba yake.

Sammy ameeleza kwamba hivi karibuni ndugu yake enzi za uhai wake, alimdokezea kwamba alikuwa anapitia hali ngumu ya kifedha.

Amesema hadi mauti yanamfika mtangazaji huyo alikiwa akifanya shughuli zake binafsi  kusambaza bidhaa na huduma mbalimbali ofisi za Kaunti ya Kilifi.

Taarifa iliyotolewa na uomgozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kilifi jana Jumatatu imethibitisha kwamba alikuwa amejinyonga.

Mwanahabari huyo alijitosa kwenye ulingo wa kisiasa baada ya kuondoka Pwani FM mwaka 2013.

Habari kuhusu kifo chake ziliripotiwa leo Jumanne na Pwani FM kupitia ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Facebook na Twitter.

“Aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha habari cha Pwani FM, Sammy Ambari maarufu kama Mtumishi ameaga dunia kwa kujitoa uhai nyumbani kwake eneo la Mkongani, Kaunti ya Kilifi,” imeeleza taarifa hiyo.

Kutokana na tukio hilo, mmoja wa waombolezaji Gilead Shuma amesema ipo haja kwa serikali kufuatilia kuongezeka matukio ya watu kujinyoinga kutokana na ugumu wa maisha.

 “Ninatoa pole kwa familia, na marehemu apumzike kwa amani. Watu wanapitia wakati mgumu, ila wakuwashirikisha wanakosa,” amesema mkazi wa Kaunti hiyo, Andrew Kipawa.

“Tukishindwa kukabili msongo wa mawazo ni vyema tutafute huduma kwa wataalamu wahusika ili tusije  kupoteza maisha,” amesema.