Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Museveni ampiga ‘stop’ Muhoozi Twitter

Muktasari:

  • Jenerali Kainerugaba mara nyingi amezua utata kutokana na maandiko yake katika mtandao wa Twitter ukiwemo ujumbe alioandika kumlaumu Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kutogombea muhula wa tatu wa uongozi wa nchi hiyo hali iliyosababisha Rais Museveni kuingilia kati.

Kampala, Uganda. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema kuwa mtoto wake, Muhoozi Kainerugaba atakaa kando kwenye mtandao wa Twitter linapokuja suala la mijadala ya mambo ya Serikali.

Hiyo ni baada ya kuibuka mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maandiko yenye utata ya Kainerugaba anayopostio kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

Jenerali Kainerugaba (48), mara nyingi amezua utata kutokana na maoni yake anayoweka kwenye Twitter ambapo hivi karibuni aliweka andiko la kumlaumu Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kutogombea muhula wa tatu wa uongozi wa nchi hiyo hali iliyosababisha baba yake kuingilia kati.

"Ataondoka Twitter,” amesema Rais Museveni katika mahojiano yaliyorushwa na KTN Jumapili.

“Twitter sio tatizo, tatizo ni kile unachoandika. Kuzungumza kuhusu nchi nyingine na siasa za upendeleo za Uganda ni jambo ambalo hapaswi kufanya na hatalifanya," ameongeza Rais Museveni.

Oktoba 5 mwaka huu, Rais Museveni aliwaomba radhi wananchi wa Kenya kutokana na andiko lililochapishwa na Jenerali Muhokozi la kumlaumu Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kutogombea muhula wa tatu wa uongozi wa nchi hiyo.

Kupitia ujumbe wake aliouchapisha katika mtandao wa kijamii Jenerali Kainerugamba aliandika;

“Shinda yangu pekee na kaka yangu mkubwa ni kwamba hakugombea muhula wa tatu. Tungeshinda kwa urahisi,” ulisomeka sehemu ya ujumbe huo.

Katika mahojiano ya Jumatatu, Museveni alimtetea mwanaye kama "Jenerali mzuri sana," baada ya kumpandisha cheo licha ya kumvua wadhifa wake kama kiongozi wa majeshi ya nchi kavu ya Uganda.

Ingawa Kainerugaba amekanusha mara kwa mara madai kwamba ana nia ya kumrithi baba yake mwenye umri wa miaka 78 lakini baadhi ya maandiko yake yanaonyesha kuwa na nia hiyo.

Oktoba 15 mwaka huu Kainerugaba aliandika kwenye Twitter akiwaambia wapinzani kuwa baada ya baba yake, atawashinda katika uchaguzi kwa kuwa Waganda wanampenda kuliko wanavyopenda upinzani.

“Kwa wapinzani wa Uganda, baada ya baba yangu, nitawashinda vibaya katika uchaguzi wowote. Waganda wananipenda kuliko walivyowahi kuwapenda ninyi,” aliandika Kainerugaba.