Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkenya aliyekamatwa na dawa za kulevya Vietnam kunyongwa kesho

Margaret Nduta Macharia (37) aliyehukumiwa kunyongwa akiwa mahakamani nchini Vietnam. Picha na Mtandao

Vietnam. Margaret Nduta Macharia (37), raia wa Kenya aliyekamatwa mwaka 2023 nchini Vietnam na dawa za kulevya kilogramu mbili za Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na mwanaume kutoka Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John.

Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika viwanja vitatu vya ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Vietnam. Viwanja hivyo ni; Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar).

Hata hivyo, Margaret akijitetea mahakamani nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku.