Mateka Israel, Hamas kuanza kuachiliwa leo

Isarel. Kikosi cha Hamas, Izzedine al-Qassam, kimethibitisha kusitisha mapigano kwa siku nne kuanzia leo Ijumaa.
Taarifa iliyotolewa na kundi hilo imesema kuwa malori manne ya mafuta na mengine 200 ya misaada yataruhusiwa kuingia ukanda wa Gaza.
Hatua zote za kijeshi za kikosi cha al-Qassam na vikosi vya Israel zinatarajiwa kusitishwa kwa siku nne.
Israel imethibitisha kuwa imepokea orodha ya watakaoachiliwa kwanza na inawasiliana na familia zao.
Mateka 13 wataachiwa kuanzia saa kumi jioni na watakaoachiwa ni wanawake na watoto ambao watakabidhiwa Shirika la Msalaba Mwekundu, lakini hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu njia yao ya kutoka Gaza.
Qatar ambeye ni msuluhisi wa mgogoro huo, imesema kuwa inatarajia wafungwa wa Kipalestina kuachiliwa lakini haikutoa maelezo yoyote kuhusu idadi.
Chini ya mpango huo, mateka 50 wataachiliwa wakati wa kusitishwa mapigano kwa siku nne.