Hamas: Mateka wako sehemu salama ndani ya Gaza

Muktasari:
- Wakati haya yakijiri, Israel imethibitisha usitishwaji huo wa mapigano kwa muda kuruhusu kuachiliwa kwa mateka na wafungwa kwa pande zote mbili, hata hivyo; haikuweka wazi siku zoezi hilo litaanza, huku ikijiapiza kuendelea na mapigano mara muda huyo utakapokoma.
Dar es Salaam. Leo Alhamisi saa nne asubuhi, wanamgambo wa Hamas wanakusudia kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda, baina yake ya Israel; huku wakibainsha kuwa mateka wao wanashikilikiwa mahala salama katika mahandaki ndani ya Gaza.
Wakati haya yakijiri, Israel imethibitisha usitishwaji huo wa mapigano kwa muda kuruhusu kuachiliwa kwa mateka na wafungwa kwa pande zote mbili, hata hivyo; haikuweka wazi siku zoezi hilo litaanza, huku ikijiapiza kuendelea na mapigano mara muda huyo utakapokoma.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC), Jeshi ya Israel (IDF) limewahi kusema kuwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas, ni pamoja na watoto 20, na kati ya watu 10 hadi 20 wenye umri zaidi ya miaka 60.
Kwa upande mwingine, IDF imewajulisha baadhi ya familia ambazo wapendwa wao wanashikiliwa mateka, huku zile ambazo ndugu zao hawajulikani waliko, zinaamini kuwa wapendwa wao ni sehemu ya watu waliochukuliwa na wanamgambo wa Hamas.
Hata hivyo kwa mujibu wa shirika hilo la habari, siyo Israel wana Hamasi ambao wametoka orodha rasmi yenye majina ya mateka hao.
BBC imesema kuwa imeweza kutambua zaidi ya watu 200 ambao walitekwa Oktoba 7, kutokana na kuchambua mtandao unaohusishwa na Hamas, machapisho katika mitandao ya kijamii na hasa kutoka kwa wanafamilia waliochukuliwa, ripoti katika vyombo vya habari vya kimataifa na kwa kuzungumza na jamaa moja kwa moja.
Imedaiwa kuwa watu 39 kati ya mateka waliotambuliwa, wana umri wa miaka 18 au chini, ambapo mtoto wa umri wa chini ya mwaka mmoja, Kfir Bib anaaminika kuwa kuwa ndiye mateka mdogo zaidi na kwamba kuna mateka 59 wa kike wenye umri wa miaka 19 au zaidi, huku mwenye umri mkuwa akiwa ni Yafa Adar (85).
Kwa upande mwingine, makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya Israel na Hamas yanatazamiwa kuona wanawake 50 na watoto wanaachiliwa huko gaza, huku wanawake na watoto 150 wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel wataachiliwa.
Kusitishwa kwa mapigano kwa siku nne pia kumekubaliwa kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza, ambapo Malori ya misaada yameoneka yakiwa kwenye foleni katika kivuko cha Gaza nchini Misri kabla ya kusitishwa mapigano hapo jana.
Katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, Israel imeruhusu mizigo 1,399 ya mizigo ya kibinadamu kuingia Gaza kupitia Misri. Kabla ya vita, wastani wa kila mwezi ulikuwa karibu na 10,000, kulingana na UN.
Hata hivyo, kama sehemu ya mapatano yaliyoingiwa kati ya Israel na Hamas, idadi kubwa ya malori yaliyobeba misaada muhimu yataruhusiwa kuingia katika eneo hilo, huku picha mbalimbali zikionyesha zinaonyesha maandalizi yanaendelea kwa mchakato huu kuanza katika upande wa Misri wa mpaka wa Rafah kuingia Gaza.
BBC imesema kuwa imekuwa ikichunguza orodha iliyotolewa na mamlaka ya Israel ambayo inatoa maelezo ya wafungwa 300 wa Kipalestina - ambao nusu yao wanatarajiwa kuachiliwa kama sehemu ya makubaliano ambayo yanajumuisha kusitisha mapigano kwa siku nne.
Chini ya masharti ya makubaliano hayo, Hamas awali ingewaachilia wanawake 50 wa Israel na watoto waliokuwa mateka huko Gaza ili kubadilishana na wafungwa 150 - vijana wa Kipalestina pamoja na wanawake watu wazima - wanaoshikiliwa katika jela za Israel.
Katika uchunguzi wa shirika hilo, inaonyesha kuwa watu 267 trakribani asilimia 89 ya walio kwenye orodha ya Wapalestina ni wanaume, kati yao, 121 (asilimia 40) wana umri wa chini ya miaka 18; huku ikielezwa kuwa watu 203 (asilimia 68), walikamatwa kati ya 1 Januari na 5 Oktoba 2023.
Imeelezwa kuwa katika wafungwa wa kiparestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel, hakuna mwanamume aliye na umri zaidi ya miaka 19 - wote walio na umri wa miaka 20 na zaidi ni wanawake.
97 waliosalia (asilimia 32) walikamatwa kabla ya 1 Januari 2023. Hakuna hata mmoja wa watu kwenye orodha alikamatwa baada ya Hamas kushambulia Israeli Oktoba 7, 2023.