Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hamas yatoa neno usitishwaji mapigano yaahidi kuachilia mateka

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa BBC, Marzouk ameliambia shilika hilo la habari kwamba wanawake, watoto na raia si sehemu ya mashambulizi ya Hamas, mazungumzo hayo yanamfanya kiongozi wa juu kuzungumza na BBC tangu mauaji ya Oktoba 7, mwaka huu.

Dar es Salaam. Kiongozi wa Hamas, Mousa Abu Marzouk amesema  kuwa ilikuwa ni vigumu kuachiliwa mateka wanaowashikilia wakati Israel ikiishambulia Gaza kwa mabomu.

Kiongozi huyo wa Hamas ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalumu na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), huku akiahidi kwamba kundi lake litawaachia mateka hao.

"Tutawaachilia. Lakini tunahitaji kusitisha mapigano," amesema kiongozi huyo wa juu wa Hamas.

Wakati takribani watu 249 wanashikiliwa kama mateka na wanamgambo wa Hamas, Wizara ya afya inayoongozwa na kundi hilo imesema kuwa watu 10,000 wameuawa tangu Israel ianze operesheni mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa BBC, hivi majuzi Marzouk alisafiri hadi Moscow kwa kile kilichoitwa ni “kujadili kuhusu watu wanane wenye uraia pacha wa Russia na Israel” ambao ni sehemu ya waliotekwa na Hamas.

Aidha, kiongozi huyo amejitenga na madai kuhusu wanamgambo wake kuua raia, akisema kuwa kundi hilo linapambana na walengwa tu.

Kwa mujibu wa BBC, Marzouk ameliambia shirika hilo la habari kwamba wanawake, watoto na raia si sehemu ya mashambulizi ya Hamas, mazungumzo hayo yanamfanya kiongozi wa juu kuzungumza na BBC tangu mauaji ya Oktoba 7, mwaka huu.

Wangeweza tu kuwaachilia mateka,  ikiwa "Waisraeli watasimamisha mapigano ili tuweze kuwakabidhi kwa Msalaba Mwekundu". Amesema 

Kwa mujibu wa Marzouk, Kiongozi wa kundi la Kijeshi la Hamas la ‘Qassam Brigades,’ Mohamed el-Deif, aliwapa amri askari wake kutoua raia.

"El-Deif aliwaambia wazi wapiganaji wake 'msiue mwanamke, msiue mtoto na msiue mzee'," amesema na kuongeza kuwa; waliua walengwa, ni majeshi au askari pekee waliuawa,’ amesema.

Na alipoulizwa iwapo mrengo wa kisiasa wa Hamas ulijua kuhusu maandalizi ya shambulio hilo, kiongozi huyo amesema kuwa mrengo huo wenye silaha "sio lazima kushauriana na uongozi wa kisiasa. Hakuna haja."

Mrengo wa kisiasa, ulio na makao yake nchini Qatar, mara nyingi hujionyesha kuwa uko mbali na vikosi vya kijeshi huko Gaza, japo mataifa ya ulaya hayaoni tofauti yoyote.

BBC imesema kuwa mahojiano hayo na kiongozi huyo, yamefanyika baada ya Israel kukataa ombi la Marekani la "kusitisha mapigano ili kuruhusu misaada ya kibinadamu" huko Gaza, ikiwa ni pamoja na kusaidia kuondolewa kwa baadhi ya mateka.

Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa mateka wote lazima waachiliwe kabla ya mapatano yoyote ya muda kuafikiwa.

Kwa upande mwingine, Marzouk amedai kuwa kundi la kisiasa la Hamas halina orodha ya wale wote anaowataja kuwa "raia wa kigeni," ambao wanashikiliwa mateka, na kwamba hata haijui maeneo walikohifadhiwa kutokana na kushikiliwa na "makundi tofauti."

Inaelezwa kuwa kuna makundi kadhaa ndani ya Gaza yakiwemo Palestina Islamic Jihad, ambayo yanafanya kazi kwa karibu na Hamas lakini yanajitegemea.

Marzouk anaamini kuwa kusitishwa kwa mapigano kunahitajika ili kukusanya taarifa na kwamba kulikuwa na vipaumbele vingine wakati eneo hilo likikumbwa na mashambulizi ya mabomu.

Imeelezwa kuwa Marzouk atakuwa na jukumu muhimu katika mzozo huo na anatajwa huenda akawa ndiye kiongozi wa kundi la Hamas katika mazungumzo ya kuwaachilia mateka hao.