Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya mtoto wa Biden yazidi kuchukua sura mpya

Mtoto wa Rais wa Marekani, Hunter Biden

Muktasari:

  • Mashtaka yanayomkabili mtoto wa Rais wa Marekani, Joe Biden yakanushwa na Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Merrick Garland.

New York. Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Merrick Garland amekanusha madai ya mwanasiasa wa Republican kuhusu mtoto wa Rais wa nchi hiyo aitwaye Hunter Biden wa Chama cha Democratic amependelewa na idara ya sheria kwa kumkubali na kuondoa uwezekano wa kufungwa gerezani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la (VOA)  inadaiwa Hunter hakulipa kodi kwa wakati, anamiliki bunduki, huku akitumia dawa za kulevya ikiwa ni kinyume cha sheria ya nchi hiyo.

Akichunguza malipo ya familia ya Biden, Mbunge wa Marekani, James Comer amesema hayo makubaliano ni ya kumpendelea mshtakiwa na kutokumchukulia hatua zisizofaa.

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amesema makubaliano hayo hayakutoa mwafaka, ikilinganishwa na mashtaka 37 ambayo idara ya sheria imewasilisha juu ya mwanasheria huyo katika wiki mbili zilizopita kwa madai ya kutumia nyaraka za siri vibaya baada ya kutoka madarakani Januari 2021.

Trump na baadhi ya Warepublican wamesema kuchukuliwa kwa hatua tofauti  ya kesi hizi nyeti za kisiasa kunaashiria mfumo wa haki wa pande mbili nchini Marekani, huku idara ya sheria ikiwapendelea wademokratiki na kufungua mashtaka makali ya jinai dhidi ya Rais huyo wa zamani wa Republican.

Trump ameongoza kwenye kura za maoni za kitaifa hasa kwa wawaniaji wa tiketi ya Republikan, wanaotaka kumtoa madarakani Rais Biden katika uchaguzi ujao wa kitaifa wa mwaka 2024.

Wakati huohuo Mwanasheria Mkuu Garland aliyeteuliwa na Biden kuwa afisa mkuu wa utekelezaji wa sheria nchini, amesema idara ya sheria anayoiongoza inafanya kazi bila kuegemea upande wowote kisiasa, pia amesema hivyo ndivyo ilivyokuwa katika kuamua kuhusu matokeo ya uchunguzi wa miaka mitano dhidi ya Hunter Biden.