Australia kupiga marufuku TikTok

Chinese social networking service TikTok's logo on a smartphone screen. Following bans of TikTok in other European countries, the French govt banned downloading and installation of TikTok among other apps on work phones.
Muktasari:
- Australia kupiga marufuku mtandao wa TikTok kwenye vifaa vya serikali, wakifuata nyayo za Marekani, Uingereza pamoja na Ufaransa.
Dar es Salaam. Australia inatarajia kupiga marufuku matumizi ya mtandao wa TikTok kwenye vifaa vya serikali kwa sababu za usalama, taifa hilo limejiunga katika orodha ya nchi zinazozuia matumizi ya mtandao huo ikiwemo Marekani, Ufaransa na Uingereza.
Kwa mujibu wa kituo cha habari Aljazeera wameeleza kuwa kuzuiwa kwa matumizi ya mtandao huo ni kutokana na kupatiwa onyo ya maofisa wa nchi za Magharibi kwamba China inaweza kutumia programu hiyo kupeleleza watumiaji na kuendesha mijadala ya umma.
Mwanasheria Mkuu wa Australia, Mark Dreyfus amesema marufuku hiyo itaanza kutekelezwa haraka iwezekanavyo wakati misamaha itaruhusiwa kwa msingi wa kesi baada ya kesi kulingana na tahadhari za usalama.
Katazo hilo linakuja huku kukiwa na wasiwasi mkubwa nchini Australia juu ya madai ya ujasusi na kuingiliwa na Beijing, ambayo ilisababisha Canberra kupitisha sheria ya kupinga uingiliaji wa kigeni na vikwazo vya kupinga makampuni ya Kichina, ikiwa ni pamoja na Huawei.
TikTok imekanusha madai kuwa programu hiyo haijawahi na haitawahi kushiriki data na serikali ya China.
Imeandaliwa na Emmanuel Msabaha, Mwananchi