Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalimu ajinyonga akidaiwa kuliwa Sh1 milioni kwenye Aviator

Polisi wakivunja dirisha kwa lengo la kwenda kutoa mwili wa Kevin Omwenga ndani ya nyumba yake. Picha na mtandao

Muktasari:

  • Marehemu Kevin Omwenga anadaiwa kukopo Ksh50,000 kutoka kwa marafiki zake ambapo inasadikika hela hizo zililiwa kwenye Aviator.

Nyamira. Mwalimu wa sekondari ya Wavulana ya Nyamira nchini Kenya, amekutwa amefariki kwa kujinyonga nyumbani kwake.

Mwalimu huyo aliyetambulika kwa jina la Kevin Omwenga mwili wake ulipatikana ndani kwake jana Alhamisi Juni 7, 2024, huku ikidaiwa kuwa alipoteza Ksh50,000 (Sh1 milioni) kwenye kamari maarufu kama aviator au kindege.

Msaidizi wa chifu wa eneo hilo, Johnson Manyara amethibitisha kifo cha mwalimu huyo wa masomo ya kemia na hisabati.

Baadhi ya walimu walidai Omwenga alipenda sana mchezo wa kamari wa aviator na alikuwa na deni kubwa ambapo alikuwa amekopa pesa  kutoka kwa wenzake, zinazodaiwa kufika Ksh50,000  (Sh1 milioni) ambazo huenda alipoteza kwenye kamari hiyo.

"Nimekusanya kutoka kwa wenzake kwamba alikopa pesa nyingi, lakini alipoteza nyingi akicheza mchezo wa Aviator," Manyara amesema.

Mkuu wa Shule, George Onkundi amesema marehemu alionekana karibu na shule hiyo Jumatano  lakini hakuripoti kazini.

“Bado hakuwa ameajiriwa na TSC, lakini alikuwa akifundisha nasi chini ya BOM kwa miaka minne iliyopita. Hakuonyesha dalili yoyote ya msongo wa mawazo,” amesema mkuu wa shule huyo.

Kulingana na mkuu wa shule, simu zilizopigwa katika simu ya Omwenga usiku wa Jumatano na Alhamisi asubuhi hazikupokelewa, na kusababisha baadhi ya walimu kumfuata kwake kumtazama.

Mkuu huyo amesema baada kufika kwake walibisha mlango bila kujibiwa, ndipo wakaamua kuchungulia dirishani na kuuona mwili wake  ukiwa umening’inia.


Imeandaliwa kwa msaada wa The Citizen Digital.