Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uzalishaji magari ya umeme Uganda mchongo kwa Tanzania

Muktasari:

  • Uganda imeanza uzalishaji wa magari ya umeme baada ya kufungua kiwanda kinachotarajiwa kuzalisha magari 5,000 kwa mwaka, yakiwemo mabasi ya masafa marefu yanayoweza kutembea hadi kilometa 500 bila betri kuisha.

Uganda.  Wakati Uganda ikifungua kiwanda kuunganisha magari ya umeme, wadau wameeleza kuwa hatua hiyo ni fursa kwa nchi jirani ikiwemo Tanzania kupunguza matumizi ya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta kila mara.

Kiwanda hicho kwa kwanza Afrika kuzalisha magari ya umeme, Kiira Motors Coorporation (KMC), kinatarajiwa kuzalisha magari 5,000 kwa mwaka yatakayohusisha magari mabasi madogo ya abiria na yale ya masafa marefu.

Takwimu zinaonyesha Tanzania kwa mwaka Tanzania hutumia wastani wa lita bilioni 4 za mafuta ambazo gharama yake hubadilika mara kwa mara kutokana na kupanda kwa thamani ya dola na gharama za usafirishaji.

Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Joseph Priscus amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni hatua kubwa katika biashara ya usafirishaji na utekelezaji wake utakuwa na manufaa pia kwa nchi.

Akizungumza leo Agosti 16, 2024 wakati wa ufunguzi wa kiwanda hicho sambamba na maonesho ya vyombo vya moto vinavyotumia umeme, Priscus amesema endapo teknolojia ya magari ya umeme itashika kasi, itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uendeshaji na nchi itapata mapato yatokanayo na mauzo ya umeme.

Amesema Tanzania inatumia kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi hivyo endapo magari ya umeme yataanza kutumika, fedha hizo zitabaki nchini kwa ajili ya matumizi mengine.

Amesema kwa muda mrefu kumekuwa na mabadiliko katika bei za mafuta, hali inayosababisha kuyumbisha biashara ya usafirishaji, hivyo teknolojia ya gesi na umeme ni mkombozi.

“Hiki kiwanda kipo Uganda lakini sisi kama nchi jirani naona tunaweza kuitumia fursa hii na kupata manufaa. Kama nchi tunatumia fedha nyingi kuagiza mafuta lakini tukiwa na magari haya, hatuna sababu ya kutumia fedha hizo kwa sababu umeme tunao.

“Tunaona hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha tunakuwa na umeme wa uhakika, ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, hivyo nishati ya umeme tunayo ya kutosha kwa ajili ya magari haya,” amesema Priscus na kuongeza:

“Mbali na faida ambazo Serikali itapata kupitia mauzo ya umeme, kwa upande wetu wafanyabiashara magari haya yatapunguza gharama za uendeshaji kwa kuwa teknolojia hii haina matumizi makubwa ya vilainishi wala matengenezo ya mara kwa mara.”

Mkurugenzi Mkuu wa Kiira Motors, Paul Musasizi amesema Serikali ya Uganda imetumia dola 85 milioni (Sh230 bilioni) kufanya uwekezaji huo unaoenda kuifanya kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki na kati kuwa kiwanda cha kutengeneza  magari ya umeme.

Amesema tayari kiwanda hicho kimeshazalisha magari 40 ambayo yameanza kutoa huduma ya kubeba abiria katika miji ya Entebe, Jinja na Kampala.

Amesema mpango wa kuwa na kiwanda hicho ulianza 2007 kwa kupeleka wataalamu nje kujifunza tekinolojia hiyo na hatimaye waliweza kutengeneza magari hayo nchini Uganda kupitia kiwanda kidogo, kabla ya kuanzisha kiwanda kikubwa ambacho kitazinduliwa Oktoba mwaka huu.

“Changamoto ni nyingi, mwanzo ni mgumu lakini baada ya muda watu wataelewa, dunia iliko sasa na inakoelekea suala la mazingira linapewa kipaumbele na magari haya ni rafiki wa mazingira, sisi tumeanza kutengeneza wenyewe bila shaka wengine watafuata,” amesema Musasizi.

Musasizi amesema Tanzania pia ina nafasi kubwa ya kunufaika kwenye maeneo mengi katika mnyororo wa thamani kutokana na rasilimali mbalimbali zinazotumika kutengeneza magari hayo.

Manufaa haya yanaweza kupatikana kwenye eneo la madini ya kimkakati hasa madini aina ya nickel, copper, cobalt na mengineo ambayo ni malighafi muhimu kwa ajili ya kutengeneza betri za kuchajia magari ya umeme.

Akizungumzia maonyesho hayo yanayofahamika E-mobility amesema expo ni fursa ya kukutanisha wadau mbalimbali kutoka kwenye sekta ya usafirishaji, watunga sera na wawekezaji ili waweze kuona magari hayo na kuwekeza kwenye teknolojia hiyo.


Kama una maoni kuhusu habari hii, tuandikie ujumbe kupitia WhatsApp: 0765864917.