Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge alalamikia riba kubwa kwa wakopeshaji

Muktasari:

  • Mbunge huyo pia amezungumzia namna ambavyo Serikali inachelewesha malipo kwenye tenda jambo linalowafanya wafanyabiashara wafilisike kutokana na kudaiwa madeni makubwa.

Dodoma. Mbunge wa Kigoma mjini, Kilumbe Ng’enda ameitaka Serikali kutoa tamko la lini itafanya marekebisho ya riba kwenye mikopo kwani inawaumiza Watanzania.

Kilumbe amesema wafanyabiashara na wanaolisha tenda mbalimbali kwenye taasisi za umma wanafilisika kwa sababu ya ongezeko la madeni na riba ambalo lipo kwenye taasisi za kifedha.

Ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye hotuba ya waziri mkuu katika makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/26 ambapo ofisi ya waziri mkuu iliomba kupitishiwa Sh782.08 bilioni.

“Serikali ielekeze kwa Benki Kuu (BoT), riba ni kubwa inaumiza wananchi na wafanyabiashara kwa nini isipewe nguvu BoT ili kusudi itoe ahueni kwa watumiaji wa taasisi za kifedha hasa wanaokwenda kukopa,” amesema Kilumbe.

Amezungumzia jinsi wafanyabiashara wanavyopata taabu akisema kuwa wanakopa kwa riba kubwa lakini hata huko ambako wanasambaza bidhaa zao,  Serikali inachelewa kuwalipa hivyo wanajikuta wakiendelea kupata hasara.

Ametaja eneo lingine ambalo Watanzania wanapata tatizo ni kwenye taasisi za kifedha, kwani zimekuwa zikikopa kwa riba ya asilimia 12 hadi 14 kwa mwaka kishwa wanakwenda kuwakopeshwa wananchi kwa riba ya asilimia 18 hadi 20 kwa mwezi, hivyo kwa mwaka mmoja wanakuwa wamechukua fedha nyingi za wananchi ambao ameutaja ni sawa na wizi.

Katika hatua nyingine mbunge huyo amezungumzia suala la leseni za waendesha pikipiki (bodaboda) akitaka bei yake ipungue kutoka Sh70,000 ya sasa na kuwa Sh20,000 ili Serikali ikusanye mapato ya kutosha.

Kwa mujibu wa Kilumbe, inakadiriwa kuwa wapo waendesha bodaboda zaidi ya milioni mbili, lakini wenye leseni ni asilimia ndogo huku kundi kubwa ni waendesha vyombo hivyo wasiokuwa na leseni.