Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marufuku kulipa kwa kutumia dola huduma hizi

Muktasari:

  • Hata hivyo katazo hilo haliwahusu wanaohusika na mauzo na manunuzi ya nje ikiwemo tenda kubwa za Kimataifa.

Dodoma. Serikali ya Tanzania imepiga marufuku matumizi ya malipo kwa sarafu isiyo ya Tanzania kwa madai ni moja ya njia za utakatishaji fedha.

Hata hivyo, katazo hilo haliwahusu wanaohusika na mauzo na manunuzi ya nje ikiwemo zabuni kubwa za Kimataifa.

Agizo hilo limetolewa leo Alhamisi Juni 25, 2026 na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Suma Fyandoma.

Katika swali lake kwa Waziri Mkuu, Fyandomo ameuliza nini kauli ya Serikali kuhusu baadhi ya wafanyabiashara wenye hoteli, wauzaji wa viwanja na wanaopingisha nyumba ambao wanaendelea kutoza gharama kwa kutumia Dola.

Mbunge huyo amelalamikia alichokiita watu wanajificha kwa kutoza Dola lakini wakishazibadiri kwa shilingi ya Tanzania inakuwa ni gharama kubwa.

Waziri Mkuu amesema tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kutoza malipo kwa salafu isiyo ya Tanzania ni kama ulimbukeni wa kujificha kwenye ukoloni ambao ulishapitwa na wakati.

Amesema matumizi ya malipo ya namna hiyo ni kuvunja sheria ambayo baadhi wanafikiria mawazo ya kikoloni ya kutawaliwa.

"Wengine wanatumia njia hiyo kutakatisha fedha, nitoe wito kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na vyombo vingine kutoa elimu kwani jambo hili lipo kisheria na kikatiba, ipo siku Serikali itakunjua makucha yake," amesema Waziri Mkuu.

Dk Mwigulu ametaka malipo yote ikiwemo kunukuu bei na matangazo ikiwemo kuuziana kwamba lazima yawe kwa salafu ya shilingi ya Tanzania ikiwemo hata malipo ya ada za shule.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amepiga marufuku ubadirishaji wa matumizi ya ardhi ikiwemo maeneo ya wazi ambayo yanachukuliwa na viongozi bila kufuata utaratibu.

Awali, Mbunge wa Moshi Mjini (CCM), Ibrahim Shayo ameuliza Serikali inachukua hatua gani kwa baadhi ya viongozi katika Manispaa ya Moshi ambao wamevamia maeneo ya wazi na kuanzisha ujenzi wa vibanda.

Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Ardhi kusimamia jambo hilo katika mikoa yote na isiruhusu mpango huo labla kama maeneo hayo yalitengwa kwa ajili ya kufanya maendelezo kwa siku za usoni.

"Natambua kumekuwepo na hali hiyo ya kubadirisha matumizi kinyemela na kusababisha mizozo isiyokuwa na maana na wakati mwingine kusababisha mafuriko, tuache tamaa hawa wazee wetu hawakuwa na tamaa ndiyo maana walitenga maeneo hayo," amesema Dk Mwigulu.

Kuhusu ujenzi unaoendelea katika Manispaa ya Moshi amesema Serikali itafuatilia na kujua uhalisia na nani aliruhusu kufanya hivyo.