Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii hapa sababu bei ya nyama kushuka

Dodoma/mikoani. Upungufu wa mvua katika mikoa ya Kati ya Dodoma na Singida umesababisha kilio kwa wafugaji baada ya kulazimika kuuza mifugo yao kwa wingi na kwa bei ndogo.

Kutokana na hali hiyo, bei ya nyama katika masoko na mabucha mbalimbali imeshuka kutokana na wingi wa mifugo iliyonunuliwa kwa mkupuo.

Mathalan, jijini Dodoma bei ya kitoweo hicho imeshuka kutoka Sh12,000 kwa kilo hadi Sh9,000, wakati Singida imeshuka kutoka Sh12,000 hadi Sh10,000 kwa kilo moja. Hali kama hiyo imeshuhudiwa pia katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo, wakati bei ikishuka na kuwepo kwa dalili za kushuka zaidi, kwa baadhi ya mikoa inaonekana ama kupanda au kusalia ya siku zote.

Wingi wa mifugo inayopelekwa kwenye minada umetokana na kupungua kwa ubora wa mifugo hiyo kutokana na kukosekana kwa nyasi za kutosha kwenye maeneo mbalimbali vijijini.

Kwa mfano, katika eneo maarufu la Mnada wa Msalato, bei ya nyama imeshuka huku wauzaji wakilia kupungua kwa walaji pia.

“Bei imeshuka kweli, lakini wateja tunaona wamepungua, halafu watu wanasingizia hii sikukuu. Si kweli, na mimi huu ni mwaka wa 19 nikifanya biashara hii, na hizo sikukuu huwa zipo lakini mambo yanakuwa mazuri,” amesema John Nghwasa.

Nghwasa, ambaye anamiliki bucha kadhaa jijini Dodoma na Kibaigwa, anataja sababu ya kushuka kwa bei ya nyama kuwa ni kupungua ubora wa minofu ya nyama, kwani baadhi ya maeneo nyasi hazipo kutokana na uchache wa mvua, jambo linalowalazimu baadhi ya wafugaji wenye makundi makubwa kuanza kuhamisha mifugo yao.

Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, wafugaji wameingiwa na hofu juu ya ukosefu wa malisho, hivyo wanauza mifugo yao kwa lengo la kupunguza makundi ya ng’ombe ili wasipate hasara zaidi, na hiyo ndiyo sababu ya kushuka kwa bei.

“Kafanye utafiti kidogo minadani utaona, ng’ombe ambaye mwezi Januari na Februari tulimnunua Sh1 milioni, hivi sasa anauzwa kati ya Sh800, 000 au na kidogo hivi. Hakuna uchawi, hiyo ndiyo sababu ya kushuka kwa bei ya nyama, maana watu wanakuwa na mifugo mingi kwenye mazizi yao inayosubiri kuchinjwa,” anasema John.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Singida, Ramadhan Ngaa amesema alikuwa mtu wa mwisho kushusha bei ya nyama, ingawa wenzake walianza kushusha tangu mwanzoni mwa Februari.

Ngaa anasema kwa sasa kinachowaokoa ni nyama wanazolisha tenda kwenye shule na mahoteli, ambako wanaendelea kuuza kwa Sh12, 000, lakini wakigundua nao inakuwa tatizo, nao watataka bei ishuke chini.

Mamalishe wa Soko la Sabasaba jijini Dodoma, Zubeda Othman amesema bucha nyingi hivi sasa zinaamua kukopesha nyama kwa mamalishe ili wakiuza jioni ndipo warudishe fedha, kwani suala la kuuza kwa taslimu limekuwa gumu.

Zubeda anaeleza kuwa, huenda bei ikapanda wiki ijayo kutokana na sikukuu ya Idd, lakini baada ya hapo anaamini itaendelea kushuka zaidi kwani dalili zinaonekana wazi.

Mweka hazina wa Chama cha Wafugaji wa Kata ya Nzuguni, Ernest Kutoka amesema mifugo mingi, hasa ng’ombe, kwa sasa haiko kwenye afya nzuri licha ya kuwa mvua zimeanza kunyesha na kuleta tumaini la kupata nyasi na akuwa mfugaji ndiye anaumia.

 “Ukikuta nyama inapungua buchani, lazima ujue kuwa anayekwenda kuumia zaidi ni mfugaji. Hapo lazima minadani mifugo ipungue bei, na ndivyo ilivyo sasa kwani kila mmoja analia. Kikubwa tunaona chanzo ni ukame wa malisho,” amesema Kutoka.

Mwenyekiti wa Utunzaji wa Mazingira na Ufugaji wenye Tija Tanzania, Jeremiah Wambura, amesema sababu kuu ya kushuka kwa bei ya nyama sokoni ni kutokana na watu kutokufuata ushauri wa kufuga kitaalamu.

Wambura anakiri mifugo inapitia changamoto kubwa ya ukosefu wa maji, na katika sehemu nyingi afya za mifugo siyo nzuri, jambo linalopelekea watu kuwa na hofu na hivyo kuanza kuuza hata ng’ombe ambao hawakuwa wamepanga.

Anasema wafugaji wengi hawana utamaduni wa kuhifadhi nyasi kwa ajili ya akiba ya chakula cha mifugo hata mvua zinapokuwa nyingi, hivyo inawapa wakati mgumu wanapofikiria watapeleka wapi mifugo yao kila sehemu ikionekana kutokuwa na malisho, badala yake wanaanza kuuza kwa bei ya chini.

“Ni kweli hali ya hewa si nzuri kwa mifugo, ng’ombe hawana afya nzuri, lakini mnasahau kuwa kumekuwepo na viwanda vingi vya nyama, ambavyo vinafanya kuwepo kwa soko la ushindani na udalali. Ukichanganya haya yote, kwa nini bei isishuke?” amehoji.

Mfugaji huyo ametahadharisha kuwa hali inakoelekea huenda bei ya nyama itashuka zaidi, kwani miezi michache ijayo kipaumbele kitakuwa si nyama, badala yake watu wataelekeza nguvu kwenye manunuzi ya chakula, hivyo bucha za vijijini zipo kwenye hatari ya kufungwa.

Tofauti na kwenye mikoa hiyo, jijini Mbeya bei ya nyama imeongezeka kutoka Sh9,000 kwa kilo moja hadi Sh10,000, huku sababu ikitajwa ni uhaba wa ng’ombe kwenye masoko na minadani na hivyo kuuzwa bei ya juu.

Katika mikoa ya Kilimanjaro na Morogoro, bei ya kilo moja ya nyama imebaki Sh12, 000, wakati Zanzibar nyama inauzwa kwa Sh15, 000 kwa kilo moja.

Hata hivyo, taarifa iliyochapishwa Machi 24, 2025 na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Kitengo cha Bodi ya Nyama, inaonyesha Mnada wa Pugu pekee ndio ambao bei ya ng’ombe hai iliuzwa kwa bei ya juu kidogo, ukilinganisha na maeneo mengine ya minada nchini.

Taarifa hiyo inaonyesha wastani wa bei ya kilo moja ya ng’ombe hai iliuzwa kati ya Sh10, 000 hadi wastani wa Sh8, 500, badala ya wastani wa Sh11, 000 na Sh9, 600.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa bei hizo zilirekodiwa hadi Machi 14, ikiwa imeshuka kwa wastani wa asilimia 8.3 hadi asilimia 12.5.

Imeandikwa na:
Habel Chidawali (Dodoma), Jesse Mikofu (Zanzibar), Hamida Shariff (Moro), Hawa Mathias na Saddam Sadick (Mbeya), Janeth Joseph (Moshi).





John ambaye anamiliki bucha kadhaa jijini Dodoma na Kibaigwa, anataja sababu kuu ya kushuka kwa bei ya nyama kwamba inasababishwa na ubora minofu ya nyama kwani baadhi ya maeneo nyasi za kuchungia mifugo hazipo kutokana na uchache wa mvua jambo linalowalazimu baadhi ya wafugaji wenye makundi makubwa kuanza kuhamisha mifugo yao.

Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, wafugaji wameingiwa na hofu juu ya ukosefu wa malisho hivyo wanauza mifugo yao kwa lengo la kupunguza makundi ya ng’ombe na ndiyo inakuwa sababu ya kushuka kwa bei.

“Kafanye utafiti kidogo minadani utaona, ng’ombe ambaye mwezi Januari na Februari tulimnunua Sh1 milioni, hivi sasa anauzwa kati ya Sh800,000 au na kidogo hivi, hakuna uchawi hivyo ndiyo sababu ya kushuka kwa bei ya nyama maana watu wanakuwa na mifugo wengi kwenye mazizi yao wanaosubiri kuchinjwa,” anasema John.

Akizungumza kwa njia simu kutoka Singida, Ramadhan Ngaa anasema alikuwa mtu wa mwisho kushusha bei ya nyama ingawa wenzake walianza kushusha tangu mwanzoni mwa mwezi Februari.

Ngaa anasema kwa sasa kinachowaokoa ni nyama ambazo wanalisha tenda kwenye mashule na mahoteli ambako huko wanaendelea kuuza kwa Sh12,000 lakini wakigundua nao inakuwa tatizo na wao watataka bei ishushe chini.

Mama lishe wa soko la sabasaba jijini Dodoma Zubeda Othman amesema bucha nyingi hivi sasa wanaamua kukopesha nyama kwa mama lishe ili wakiuza jioni ndipo warudishe fedha kwani suala la kuuza kwa taslim limekuwa gumu.

Zubeda anaeleza kuwa, huenda bei hizo zikapanda wiki kesho kutokana na sikukuu lakini baada ya hapo anaamini kuwa zitaendelea kushuka zaidi kwani dalili zinaonekana wazi.

Muweka hazina wa Chama cha Wafugaji wa Kata ya Nzuguni Ernest Kutoka anasema mifugo mingi hasa ng’ombe kwa sasa haiku kwenye afya nzuri licha ya kuwa mvua zimeanza kunyesha na kupeleka tumaini tena la kupata nyasi.

Kutona amekiri bei ya nyama kupungua kwenye mabucha kunakopelekea wanunuzi wa mifugo nao kushusha bei hizo minadani.

“Ukikuta nyama inapungua buchani lazima ujue kuwa anayekwenda kuumia zaidi ni mfugaji, hapo lazima minadani mifugo ipungue bei na ndivyo ilivyo sasa kwani kila mmoja Analia kikubwa tunaona chanzo ni ukame wa nyasi kwenye malisho,” amesema Kutoka.

Wakati Dodoma na Singida bei ikishuka, Jijini Mbeya bei ya nyama imeongezeka kutoka Sh9,000 kwa kilo moja hadi Sh10000 huku sababu ikitajwa ni uhaba wa ngo’mbe kwenye masoko na minadani.

Sababu kuwa kwenye kitoweo hicho inatajwa kuwa minada ambayo imekuwa na mifugo wengi hivi sasa wanunuzi wamekuwa ni wengi lakini mifugo ni michache hivyo wanalazimika kununua kwa bei ya juu.

Katika mikoa ya Kilimanjaro na Morogoro bei ya kilo moja ya nyama imebaki Sh12,000 wakati Zanzibar nyama inauzwa kwa Sh15,000 kilo moja.

Mwenyekiti wa Utunzaji wa Mazingira na Ufugaji wenye tija Tanzania Jeremiah Wambura yeye amesema sababu kuu ya kushusha kwa bei ya nyama sokoni ni kutokana na watu kutokufuata ushauri wa kufuga kitaalamu.

Wambura anakiri mifugo inapitia kwenye changamoto kubwa ya ukosefu wa maji na sehemu nyingi afya za mifugo siyo nzuri jambo linalopelekea watu kuwa na hofu na hivyo kuanza kuuza hata wale ambao hawakuwa wamepanga kufanya hivyo.

Anasema wafugaji wengi hawana utamaduni wa kuhifadhi nyasi kwa ajili ya akiba ya chakula cha mifugo hata mvua zinapokuwa nyingi hivyo inawapa wakati mgumu w akuwaza sasa watapeleka wapi kila sehemu kunaonekana kutokuwepo kwa malisho badala yake wanaanza kuuza kwa bei ya chini.

“Ni kweli hali ya hewa siyo nzuri kwa mifugo, ng’ombe hawakuwa na afya nzuri lakini mnasahau kuwa kumekuwepo na viwanda vingi vya nyama ambavyo vinafanya kuwepo kwa soko la ushindani na udalali ukichangiwa kwa nini bei isishuke,” anasema.

Mfugaji huyo anatahadharisha kuwa hali inakoelekea huenda bei ya nyama itashuka zaidi kwani miezi michache mbele kipaumbele kitakuwa siyo nyama badala yake watu wataelekeza nguvu kwenye manunuzi ya chakula hivyo bucha za vijijini kuna hatari zikafungwa.

Katika taarifa iliyochapishwa Machi 24,2025 inaonyesha mnada wa Pugu pekee ndio ambao bei ya ng’ombe hai aliuzwa kwa bei ya juu kidogo ukilinganisha na maeneo mengine kwenye minada nchini.

Taarifa hiyo ambayo imechapishwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kitengo cha Bodi ya nyama, kinaonyesha wastani wa bei ya kilimo moja ya ng’ombe hai iliuzwa kati ya Sh1,000 hadi wastani wa Sh8500 badala ya wastani wa Sh11000 na Sh9600.

Ripoti hiyo inaonyesha bei hizo ni hadi Machi 14  ambapo zimeshuka kwa wastani wa asilimia 8.3 hadi asilimia 12.5.


Imeandikwa na Habel Chidawali (Dodoma), Jesse Mikofu (Zanzibar) Hamida Shariff (Moro), Hawa Mathias na Saddam Sadick (Mbeya) Janeth Joseph (Moshi).