Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

GIZ, TanTrade zawatangazia fursa wanawake na vijana

Muktasari:

  • Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Shirika la ushirikiano wa kimataifa la Ujerumani (GIZ) zimetangaza ushirikiano wa kuwawezesha wanawake na vijana nchini kwa kuwatafutia fursa za kibiashara ndani na nje ya Tanzania.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Shirika la ushirikiano wa kimataifa la Ujerumani (GIZ), zimekubaliana kushirikiana katika uwezeshaji wa sekta ya biashara hususan eneo la wafanyabishara wanawake na vijana wanaovuka mipaka.

 Pia, TanTrade na GIZ zimeonesha nia hiyo hivi Mei 8, 2023 ya kushirikiana eneo muhimu la taarifa za biashara na kurahisisha wafanyabiashara kuzipata kwa njia rahisi.

Kaimu Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa TanTrade, Fortunatus Mhambe alisema uwezeshaji huo unalenga zaidi miradi ya maendeleo kwa wafanyabiashara wajasiriamali wadogo waliopo maeneo ya mipakani ili kuwarahisishia kufanya biashara kwa ufanisi.

Alisema itakuza biashara zao na uchumi kwa ujumla pamoja na kuwezesha kwenye ukusanyaji wa hatua za uingizaji na uuzaji wa mazao na bidhaa mbalimbali nje ya nchi kwenye Mfumo wa Trade Information Portal.

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi kutoka GIZ, Claudia Hofmann alisisitiza nchi ya Ujerumani ipo tayari kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Tanzania kwa kuwawezesha wafanyabiashara wadogo waliopo mpakani hususan wanawake na vijana hivyo imekuja na mpango mkakati wa kuwasaidia wafanyabiashara hao kwa kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zao kwa uhuru na ufanisi zaidi.

“Programu  hii inalenga kukuza biashara ndani na nje ya Tanzania, tumejipanga kutoa mafunzo na kuwapa wadau wetu nafasi za kuonesha bidhaa zao, kuwajengea uwezo wa kufanya biashara kwa uhuru na ufanisi  zaidi na tunatoa nafasi kwa wadau kupata masoko mbalimbali ya ndani na nje ya nchi,” alisema