Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC atoa onyo kwa wanaovamia wawekezaji kwa mishale Babati

Mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara,   Emmanuela Kaganda, akizungumza wakati akisuluhisha mgogoro wa ardhi wa baadhi ya wakazi wa vijiji vya Kiru, Masware na Malangi na mwekezaji wa Dudumela plantation. Picha na Joseph Lyimo

Muktasari:

  • Baadhi ya wakazi wa vijiji vya Kiru, Masware na Malangi, wilayani Babati mkoani Manyara, wamevamia na kulima na kujenga kwenye eneo la shamba la mwekezaji wa kampuni ya Dudumela plantation.

Babati. Mkuu wa Wilaya ya Babati, Manyara, Emmanuela Kaganda amewataka baadhi ya wakazi wa vijiji vya Kiru, Masware na Malangi waliojenga makazi yao ndani ya eneo la mwekezaji kubomoa nyumba zao ndani ya siku Moja na kuacha eneo Hilo likiwa wazi

DC Kaganda ametoa maelekezo hayo Aprili 24, 2026 mara baada ya kufika katika vijijji hivyo vyenye mgogoro wa ardhi na mwekezaji wa kampuni ya Dudumela plantation.

Mgogoro baina ya wananchi hao wa vijiji hivyo vitatu na mwekezaji huyo wa Dudumela Plantation ni wa muda mrefu na umekuwa ukisababisha taharuki na sintofahamu baina ya pande hizo mbili.

Akizungumza kwenye mkutano hadhara uliowakutanisha wakazi wa vijiji hivyo na mwekezaji, Kaganda amewataka wananchi hao waliovamia kuondoka na kwenda kujenga sehemu iliyo rasmi.

Mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara,   Emmanuela Kaganda, akizungumza wakati akisuluhisha mgogoro wa ardhi wa baadhi ya wakazi wa vijiji vya Kiru, Masware na Malangi na mwekezaji wa Dudumela plantation. Picha na Joseph Lyimo

Amewataka wananchi kuacha vitendo vya kupiga wawekezaji hao kwa mishale pindi wakiwa kwenye shughuli zao kitendo ambacho ni uvunjifu wa amani kwenye eneo hilo.

"Mtu yoyote akijaribu kufanya hivyo hatua za kisheria dhidi yake zitachukuliwa kwani mnasababisha uvunjifu wa amani na mwekezaji anashindwa kulima na kufanya shughuli zake sababu ya baadhi ya watu," amesema DC Kaganda.

Hata hivyo, ameagiza wawekezaji hao kuachia baadhi ya maeneo ili wakazi wa eneo hilo waendelee kufanya shughuli za makazi na kilimo na kuepusha migogoro ya ardhi ya kila mara.

"Mwekezaji ataachia ekari 30 ambazo mtapewa bure ili kuepusha migogoro ya kila mara na endapo nitasikia kuna mgogoro tena nitachukua hatua kali dhidi ya wanaoianzisha," amesema DC Kaganda.

Amewaagiza baadhi ya watu waliojenga nyumba kwenye maeneo yenye mgogoro kuziondoa nyumba hizo na kwenda kuzijenga maeneo mengine.

Baadhi ya wakazi wa vijiji vya Kiru, Masware na Malangi wilayani Babati mkoani Manyara, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo Emmanuela Kaganda akizungumza nao juu ya mgogoro wao na mwekezaji wa Dudumela plantation. Picha na Joseph Lyimo

"Ofisa mtendaji wa kijiji na kata simameni hilo watu waliojenga maeneo yenye mgogoro hakikisheni wameondoa matofali yao na kwenda kujenga sehemu zisizo na migogoro," amesema DC Kaganda.

Mmoja kati ya wakazi wa vijiji hivyo, Magdalena Julius amesema wamejenga nyumba zao baada ya kuruhusiwa na viongozi wa viongozi wao kujenga makazi katika maeneo hayo.

"Kwa sababu sisi tumefika maeneo haya kwa muda mrefu tukapewa idhini ya kujenga na sisi tunajenga ili kupata maelezo ya kuishi," amesema.