Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afrika Kusini kuwekeza uzalishaji umeme wa nyuklia

Muktasari:

  • Serikali ya Afrika Kusini inakusudia kujenga mitambo ya nyuklia kwa ajili ya kuzalisha megawati 2,500 za umeme.

Johannesburg. Wakati Afrika Kusini ikiendelea kupambana na changamoto ya kukatika kwa umeme, Serikali ya nchi hiyo imebainisha kuwa,  inakusudia kujenga mitambo ya nyuklia kwa ajili ya kuzalisha megawati 2,500 za umeme.

 Nchi hiyo ina kituo pekee cha nishati ya nyuklia barani Afrika lakini kinu hicho cha Koeberg kilichopo karibu na Cape Town, kwa sasa kinafanya kazi kwa takribani nusu ya uwezo wake.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Nishati ya Nyuklia katika Wizara ya Nishati,  Zizamele Mbambo  amewaambia waandishi wa habari kuwa, mitambo mipya ya kwanza itaanza kutumika mwaka 2032 au 2033.

Kwa mujibu wa AFP, mkurugenzi huyo amesema Afrika Kusini tayari ilikuwa imewataka wachuuzi tofauti kupeleka mapendekezo yao.

Waziri wa Umeme wa Afrika Kusini, Kgosientsho Ramokgopa amesema ziada ya megawati 2,500 za nishati ya nyuklia itakuwa hatua ya Serikali kumaliza changamoto inayoikabili nchi hiyo ya uhaba wa umeme.

Kukatika kwa umeme kwa hadi saa 12 kwa siku katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, kumeathiri vibaya uchumi na sifa ya Serikali inapoelekea kwenye uchaguzi mwaka ujao.

Kampuni ya Taifa ya Umeme ya Eskom imegubikwa na ufisadi na matatizo ya matengenezo ambayo yamesababisha kukatika kwa umeme.

Katika jitihada za kurefusha maisha ya kinu cha Koeberg kwa miaka 20, mtambo mmoja ulifungwa kwa takriban mwaka mmoja uliopita na mtambo wa pili ulifungwa kwa matengenezo wiki hii.