Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yaliyopo nyuma picha ya Tupac usiku aliopigwa risasi 

Muktasari:

  • Picha hiyo ilipigwa kama utani na mwanafunzi kutoka Chuo cha Filamu UCLA aitwaye Leonard Jefferson ambaye baada ya tukio la shambulio alishikiliwa mara kadhaa na polisi kwa ajili ya kutoa ushahidi huku camera yake ikiwa chini ya polisi

Marekani, Moja ya picha ambayo haiweze kusahaulika na imejizolea umaarufu baada ya kifo cha Tupac ni ile akiwa kwenye gari, ambayo ilipigwa saa chache kabla ya shambulio la risasi.

Picha hiyo ilipigwa kama utani na mwanafunzi kutoka Chuo cha Filamu UCLA aitwaye Leonard Jefferson ambaye baada ya tukio la shambulio alishikiliwa mara kadhaa na polisi kwa ajili ya kutoa ushahidi huku camera yake ikiwa chini ya polisi.

Moja ya jambo alilolizungumza Jefferson kwenye vyombo vya habari ni usiku huo wa tukio Tupac alikuwa mtu mwenye furaha na ndiyo maana ilikuwa rahisi kukubaliwa apige picha hiyo.

Baada ya kupigwa picha hiyo dakika chache risasi zilirindima na kumjeruhi Tupac hadi kukimbizwa Kituo cha afya Chuo Kikuu Nevada, ‘rapa’ huyo alipigania uhai wake kwa siku kadhaa na hatimaye Septemba 13,1996 alipoteza maisha kutokana na majeraha mabaya aliyoyapata kwa risasi.


                 

Ikumbukwe kuwa Septemba 7, 1996, ilianza kama usiku wa sherehe huku jiji la Las Vegas lilikuwa na shauku kuhusiana na pambano la Mike Tyson dhidi ya Bruce Seldon, lakini usiku huo uligeuka kutoka sherehe hadi kuwa mojawapo ya siku za giza zaidi katika historia ya hip-hop.