Wolper arusha dongo, mastaa waliogombana kisa Uchaguzi
Muktasari:
- Jacqueline Massawe ndilo jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa kule kwao Moshi mkoani Kilimanjaro, lakini wadau wa filamu Afrika Mashariki wanamtambua kama Jacqueline Wolper, hivi sasa akiwa mama wa watoto wawili wazuri.
Dar es Salaam. Staa wa Bongo Movies na mjasiriamali Jacqueline Wolper amewataka wasanii wenzake waliotofautiana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, mwaka huu kumaliza bifu kwani zoezi hilo limemalizika na maisha lazima yaendelee.
Akipiga stori na Mwananchi, Wolper amesema anamshukuru Mungu yeye hakuwa na bifu na mtu kwa sababu alijua kabisa kuna maisha baada ya uchaguzi ila wapo ambao waliingia katika migogoro ya kisiasa kwa tofauti za kiitikadi.
“Jamani wasanii wenzangu mliotofautiana na kuwekeana bifu kipindi cha uchaguzi, nawasihi mmalize ili tufanye kazi kwa bidii kwani wakati wote wa kampeni tasnia ya filamu ilikuwa imelala, na mambo mengine nje ya sanaa yalilala kiasi chake,“ amesema Wolper.
Wolper alipata umaarufu kupitia filamu iliyoitwa Tom Boy na kisha Dereva Taxi, Ama Zao Ama Zangu na nyingine nyingi pamoja na tamthilia za luninga.
Jacqueline Massawe ndilo jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa kule kwao Moshi mkoani Kilimanjaro, lakini wadau wa filamu Afrika Mashariki wanamtambua kama Jacqueline Wolper, hivi sasa akiwa mama wa watoto wawili wazuri.