Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tesa wa Huba afariki dunia

Mwigizaji Grace Mapunda enzi za uhai wake

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwananchi Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Chiki Mchoma amesema mwigizaji huyo awali aliugua kwa muda mrefu kisha akarudi kwenye hali ya kawaida na kuendelea na majukumu yake kama kawaida, ndipo juzi alikimbizwa hospitalini hadi umauti ulimkuta.

Dar es Salaam. Mwigizaji Grace Mapunda maarufu kama ‘Tesa’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Novemba 2, 2024 akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi, kwenye Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Chiki Mchoma amesema mwigizaji huyo awali aliugua kwa muda mrefu kisha akarudi kwenye hali ya kawaida na kuendelea na majukumu yake kama kawaida, ndipo juzi alikimbizwa hospitalini hadi umauti ulimkuta.

"Alikuwa anaumwa akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala, kwa bahati mbaya umauti ukamkuta hapo alikuwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Hadi kufikia usiku wa kuamkia leo umauti ukamkuta, "amesema Mchoma

Hata hivyo kwa upande wake Mwigizaji menzie Jacob Stephane 'JB' amesema atamkumbuka Grace kwa ucheshi na utendaji kazi wake

"Katika waigizaji wa kike Grace alikuwa ni kati ya waigizaji wazuri na wakubwa sana, mcheshi, mara ya mwisho nilimuona jana hospitali, hatukuweza kuzungumza alikuwa ICU (Chumba cha Wagonjwa Mahututi), "amesema JB.

Naye, mwigizaji mwenzake wa tamthilia ya Huba, Rammy Galis maarufu kama ’Dev’ kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika; “MAMA 💔 … Ina Lillahi Waina Ileyhi Rajiun . Mwenyezi Mungu akusamehe  na akujaalie kile chema mama katika safari yako .

“Nilipokuona jana (ICU) , niliumia sana na sikua na uwezo wa kubadilisha hali niliyokua naiona machoni kwangu . Umenilea , umenifundisha na leo umeniacha.”

Endelea kufuatilia Mwananchi, kwa taarifa zaidi