Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali kukuza ajira kwa vijana, Sekta ya Sanaa na Burudani

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba akiwasilisha bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024 / 2025, jijini Dodoma leo Juni 13, 2024. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Hayo yamesemwa leo Alhamisi Juni 13, 2024 na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba akiwa bungeni, jijini Dodoma, wakati alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, ambapo ameeleza kuwa Serikali inampango wa kupanua ajira kwa vijana katika sekta ya Sanaa na Burudani.

Dodoma, Serikali imeweka wazi kuwa inampango wa kukuza ajira kwa vijana katika sekta ya michezo, sanaa na burudani.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Juni 13, 2024 na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba akiwa bungeni, jijini Dodoma, wakati alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, ambapo ameeleza kuwa Serikali inampango wa kupanua ajira kwa vijana katika sekta ya Sanaa na Burudani.

“Serikali ya Awamu ya Sita inatambua umuhimu wa michezo, sanaa na burudani katika kukuza ajira hususani kwa vijana. Kwa kuzingatia hilo, Serikali imeendelea kuwaunganisha wasanii wa Tanzania na soko la kimataifa mbalimbali na kuhakikisha kuwa kazi za ubunifu wao zinalindwa,” amesema 

Hata hivyo, serikali imetenga bajeti ya Sh 285.3 bilioni katika sekta ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kwa Mwaka 2024/25, huku bajeti hiyo ikiipiku ya mwaka 2023/24 ambapo ilitengewa Sh 35.4 bilioni kwa ajili ya kukuza, kuendeleza sanaa, michezo na utamaduni.