Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sasa ni rasmi zaidi ya wasanii 30 kutumbuiza Kombe la Dunia 2026

Muktasari:

  • Michuano ya Kombe la Dunia 2026, itakayofanyika katika mataifa ya Mexico, Canada na Marekani, imekusanya idadi kubwa ya wasanii wa kimataifa kiasi cha kuifanya kuwa moja ya mashindano yenye burudani kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Kombe la Dunia.

Marekani. Kwa miaka mingi Kombe la Dunia limekuwa jukwaa la mastaa wachache wa muziki kutumbuiza wakati wa ufunguzi au fainali, lakini safari hii mambo yanaonekana kuwa tofauti kabisa.

Michuano ya Kombe la Dunia 2026, itakayofanyika katika mataifa ya Mexico, Canada na Marekani, imekusanya idadi kubwa ya wasanii wa kimataifa kiasi cha kuifanya kuwa moja ya mashindano yenye burudani kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Kombe la Dunia.


Miongoni mwa nyota watakaoongoza burudani hizo ni Shakira wa Colombia na Burna Boy wa Nigeria, ambao watatumbuiza wimbo rasmi wa mashindano, Dai Dai, katika sherehe za ufunguzi zitakazofanyika Juni 11 kwenye Uwanja wa Estadio Azteca mjini Mexico City.

Mbali na wawili hao, mashabiki pia watapata fursa ya kuwaona Tyla, J Balvin, Alejandro Fernández, Belinda, Danny Ocean, Lila Downs, Mana pamoja na Los Angeles Azules wakitumbuiza katika sherehe hiyo.

Burudani hizo hazitaishia Mexico pekee. FIFA imepanga sherehe nyingine za ufunguzi nchini Canada na Marekani, zitakazowakutanisha mastaa kama Katy Perry, Future, LISA, Rema, Anitta, Michael Buble, Alanis Morissette, Alessia Cara na Jessie Reyez.

Kana kwamba hiyo haitoshi, FIFA pia imepanga kwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia tamasha maalum la muziki wakati wa mapumziko ya fainali itakayochezwa Julai 19 mjini New York.

Tamasha hilo linatarajiwa kuwakutanisha katika jukwaa moja mastaa wakubwa duniani akiwamo Madonna, BTS na Shakira.


Hivyo zaidi ya wasanii 30 kutoka mabara mbalimbali wametangazwa kushiriki katika shughuli za ufunguzi, tamasha za maandalizi na fainali za Kombe la Dunia 2026, jambo linalofanya mashindano hayo yaonekane si tu kama tamasha la soka bali pia moja ya matukio makubwa zaidi ya muziki duniani.

Iwapo ratiba hiyo itakamilika kama ilivyopangwa, Kombe la Dunia 2026 linaweza kuweka rekodi kama moja ya mashindano yaliyowakusanya wasanii wengi zaidi kuwahi kushiriki katika historia ya mashindano hayo.

WASANII WALIOTANGAZWA KUSHIRIKI

Shakira, Burna Boy, Tyla, J Balvin, Alejandro, Fernandez, Lila Downs, Belinda,Danny Ocean, Mana, Los Angeles, Azules, Michael Buble, Alanis Morissette, Alessia Cara, Jessie, Reyez, William Prince, Nora Fatehi.

Elyanna Vegedream, Sanjoy, Katy Perry, Future, LISA, Anitta, Rema, Davido, Ayra Starr, Major Lazer, Daddy Yankee, Shenseea, Madonna pamoja BTS kutoka nchini