Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

P Diddy na kashfa ya kusikitisha

Ulimwengu wa burudani ulitikiswa sana mwezi huu wakati habari za "kashfa ya P Diddy" zilipochapishwa kwenye vyombo vya habari, hususani mitandao ya kijamii, zikivuta hisia za mashabiki na wakosoaji kwa pamoja.

Kashfa hii inayomhusisha Sean Combs, anayejulikana zaidi kama P Diddy, imezua utata kuchochea mijadala kwenye majukwaa ya habari.

P Diddy, jina linalohusishwa na hip-hop na ujasiriamali, amekuwa akitamba sana katika tasnia ya muziki kwa miongo kadhaa, lakini sasa kashfa za hivi karibuni zimezua mashaka juu ya kazi yake iliyotukuka, ikiibua maswali mengi kuhusu taswira yake kwa umma. Kadiri hadithi hii inavyoendelea kusimuliwa, mashabiki wanabaki katikati ya msanii wanayemuenzi na kashfa inayomzunguka.

Katikati ya mwezi huu wa Oktoba shtaka jipya lilifunguliwa dhidi P Diddy katika mahakama ya California, likidai kwamba alilipiza kisasi dhidi ya mwanamke aliyedai kwamba alishiriki katika kifo cha Tupac Shakur kwa kupanga atekwe nyara na kubakwa na genge la wahuni mwaka 2018.

Kashfa nyingi zilianza kuonekana kuanzia katikati ya mwaka jana, 2024, baada ya msururu wa watu kumfungulia mashtaka mahakamani wakidai kuwa walidhalilishwa kingono na rapa huyo.

Novemba 16, mwaka jana, Casandra Ventura, anayejulikana kwa jina moja kama Cassie, ambaye ni mwimbaji, mcheza dansi, muigizaji na mwanamitindo wa Marekani, alifungua shauri mahakamani dhidi ya P Diddy, akidai kuwa alimlawiti mwaka 2018 na kumfanyia vitendo vya unyanyasaji, huku akidai fidia ya dola milioni 30.

Novemba 23, mwaka huo huo, mtu mwingine ambaye hakutajwa jina alidai kuwa P Diddy na mtunzi wa nyimbo Aaron Hall mwaka wa 1990 au 1991 walimnyanyasa kingono yeye na rafiki yake walipokutana katika tamasha la MCA Records mjini New York.

Tarehe hiyo hiyo ndiyo siku ambayo mwanamke anayeitwa Joie Dickerson-Neal alidai katika kesi kwamba P Diddy alimwekea dawa za usingizi kwenye kinywaji, akambaka na kurekodi kwa siri. Alidai hiyo ni wakati akiwa mwanafunzi wa chuo mwaka 1991.

Desemba 6, mwaka huohuo wa jana, P Diddy alikabiliwa na kesi nyingine ya unyanyasaji wa kijinsia, akishutumiwa kumwekea mtu dawa za usingizi na kushirikiana na wengine kumbaka mwanamke mmoja ambaye jina lake lilifichwa. Ilidaiwa kuwa kitendo hicho kilitendeka mwaka 2003, wakati mwanamke huyo akiwa na umri wa miaka 17.

Februari 26, mwaka huu, mtayarishaji wa nyimbo, Rodney “Lil Rod” Jones, alimfungulia P Diddy kesi mahakamani mjini New York, akidai alilazimishwa na Diddy kufanya naye ngono pamoja na washirika wake.

Mei 19, mwaka huu, Cassie Ventura, aliyekuwa mpenzi wa P Diddy, alizungumza baada ya CNN kupata video ya mwaka 2016 ikionyesha P Diddy akimshambulia katika korido ya hoteli.

Mei 22, mwanamitindo wa zamani, Crystal McKinney, alifungua kesi katika mahakama ya Manhattan akimtuhumu P Diddy kumwekea dawa za usingizi katika studio yake ya kurekodia huko New York mwaka 2003, kisha akamwingilia kingono.

Siku mbili baadaye, Mei 24, mwanamke mwingine, April Lampros, alimfungulia P Diddy mashtaka jijini New York akidai kuwa alishambuliwa kingono kwenye matukio manne “ya kutisha ya kingono” kati ya mwaka 1995 na 2001, yakiwamo matukio matatu ya ubakaji na moja ambalo P Diddy alimlazimisha kutumia madawa za kulevya.

Septemba 16 P Diddy, alikamatwa huko Manhattan baada ya kushtakiwa na jopo kubwa la waendesha mashtaka.

Siku moja baadaye, Septemba 17, Mahakama mjini Manhattan ilimfungua mashtaka dhidi ya P Diddy kwa makosa ya ulaghai, biashara ya ngono na usafirishaji wa watu kwa ajili ya biashara ya ukahaba, ikidai kwamba alikandamiza, kutishia na kulazimisha wanawake na wengine waliomzunguka kutimiza tamaa zake za ngono na kuficha tabia yake.

Siku hiyo hiyo, Septemba 17, taarifa iliyowasilishwa kwa jaji wa New York, Robyn Tarnofsky, ilimshutumu P Diddy na washirika wake kwa kuteketeza gari la mtu ambaye hakutajwa jina. Tuhuma hiyo inayofanana na ile iliyowasilishwa na mpenzi wa zamani wa P Diddy, Cassie Ventura, ambaye alisema katika mashtaka aliyowasilisha mwaka jana kwamba P Diddy alilipua gari la rapa Kid Cudi.

Kesho yake, Septemba 18, mawakili wa P Diddy walitaja kile walichokiita hali "mbaya" katika Kituo cha Msaada wa Metropolitan kilichoko Brooklyn, New York, katika ombi la dhamana. Hata hivyo, ombi hilo lilikataliwa na Jaji Andrew Carter.

Kama vile haitoshi, Septemba 24, mwanamke mwingine, Thalia Graves, alifungua kesi mahakamani mjini New York akidai kwamba P Diddy alimpa glasi ya divai mwaka 2001, alipokuwa na umri wa miaka 25, ambayo ilimfanya "ajisikie kuwa na kichaa, kizunguzungu na dhaifu kimwili" kabla ya kupoteza fahamu na kubakwa na wanaume wawili huku mikono yake ikiwa imefungwa nyuma ya mgongo wake.

Mwanamume mwingine aliyetajwa katika kesi hiyo ni Joseph Sherman ambaye wakati huo alikuwa mpambe wa P Diddy katika masuala ya ulinzi.

Septemba 27, P Diddy alituhumiwa kumbaka mwanamke mmoja mara kadhaa, ambapo mwanamke huyo, aliyejulikana kama Jane Doe katika kesi hiyo, alidai pia kuwa alipata ujauzito katika tukio mojawapo la kubakwa na hivyo anadai fidia.

Septemba 30, mawakili wa P Diddy waliiomba Mahakama ya Rufaa ya New York ifute uamuzi wa kuzuia dhamana. Lakini Jaji Andrew Carter alisema masharti yoyote ya kumpa dhamana hayatoshi kupunguza hatari ya yeye kuingilia mashahidi.

Oktoba 1, mwanasheria wa Texas, Tony Buzbee, alisema anawawakilisha waathiriwa 120 wanaopanga kufungua mashtaka ya kiraia katika majimbo mbalimbali wakidai uhalifu kama vile unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji na unyanyasaji wa watoto katika madai yatakayojumuisha "watu wengi wenye nguvu" na "siri nyingi chafu" dhidi ya P Diddy.

Oktoba 10, P Diddy alionekana mahakamani kwa mara ya kwanza tangu alipotiwa mbaroni, ambapo tarehe ya kesi ilipangwa kuwa Mei 5 mwaka ujao ili akabiliane na mashtaka ya utapeli, biashara ya ngono na usafirishaji wa watu kushiriki katika ukahaba.

Oktoba 11, jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa ya Marekani walisikiliza ombi la P Diddy la dhamana, wakaamuru aendelee kubaki gerezani hadi uamuzi ufanywe.


Oktoba 14, Buzbee alifungua kesi kwa niaba ya mwanamke mmoja ambaye hakutajwa jina, ambaye anadai Diddy alimwalika yeye na rafiki yake kwenye chumba cha hoteli, ambapo alitishia "kuwaua wote wawili" akiwalazimisha wanywe pombe na kutumia dawa za kulevya na hatimaye kuwabaka". Ilidaiwa tukio hilo lilifanyika mwaka 2004; wakati huo alikuwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 19 huko Brooklyn na alikuwa amealikwa kwenye sherehe ya Diddy karibu na chuo chake.

Siku hiyo hiyo, Oktoba 14, mtu mmoja kutoka Georgia alifungua kesi jijini New York akidai kuwa alipewa kinywaji kilichotiwa dawa katika sherehe iliyoandaliwa na Diddy mwaka 2021, kilichomfanya "ashindwe kujidhibiti" na "ahisi mwili wake kulegea sana" kabla ya  wanaume watatu, akiwamo P Diddy, kumbaka.

Kabla siku hiyo haijaisha, mwanamume mmoja kutoka Ohio alifungua mashtaka mahakamani akidai kuwa mwaka 2008 P Diddy na washirika wake walimlazimisha kufanya mapenzi kwa mdomo huku P Diddy akimtishia kwa bastola akisema "nitakuuwa".


Siku hiyohiyo, mwanamke mwingine alifungua mashtaka akidai kuwa P Diddy alitaka kuzungumza naye kwa faragha katika sherehe moja mwaka 1995 kabla ya kumgonga kichwa kwenye ukuta na kumbaka, akisema, "Ni bora usimwambie mtu yeyote kuhusu hili, la sivyo nitakuua."


Siku hiyohiyo, Oktoba 14, mwanamume mmoja kutoka New Jersey alidai katika malalamiko tofauti kwamba alikuwa akifanya kazi za usalama kwenye sherehe ya "white party" mwaka 2006 alipopewa na P Diddy vinywaji viwili vyenye kilevi kabla ya "kuingizwa kwa lazima katika gari lililokuwa wazi" na kulawitiwa na P Diddy.


Oktoba 14, Mwanasheria kutoka Houston, Tony Buzbee, aliwasilisha kesi dhidi ya P Diddy ambapo mwanaume asiyejulikana kutoka North Carolina alidai kuwa alikuwa na umri wa miaka 16 na alikuwa akijaribu kuingia kwenye tasnia ya muziki alipofanyiwa vitendo vya udhalilishaji na P Diddy katika mojawapo ya matamasha ya msanii huyo huko Hamptons mwaka 1998, tukio ambalo anadai kuwa bado linaendelea kumdhalilisha na kumtia aibu.


Oktoba 15, mwanamke aitwaye Ashley Parham alifungua mashtaka dhidi ya P Diddy katika mahakama ya California, akidai kwamba alibakwa kikatili na P Diddy na washirika wake mwaka 2018 baada ya kudai kwamba alihusika na mauaji ya Shakur mwaka 1996, jambo ambalo lilimuweka kwenye mazingira ya kulipiziwa kisasi.

Lakini je, P Diddy ni nani na kwanini amekumbwa na mashtaka mengi kiasi hicho?


Tukutane toleo lijalo.