Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyumba ya Kim Kardashian yarejea sokoni

Muktasari:

  • Kim, mwanzilisha wa chapa ya mavazi ya Skims aliishi katika nyumba hiyo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 huku akiitumia katika kuandaa kipindi chake maarufu cha Keeping Up With the Kardashians.

Marekani, Mwanamitindo na staa wa vipindi vya runinga, Kim Kardashian (43) kutoka Marekani ameirejesha sokoni nyumba yake iliyopo mji wa kishua Beverly Hills, Los Angeles na sasa anahitaji kiasi cha Dola5.1 milioni.

Kim, mwanzilisha wa chapa ya mavazi ya Skims aliishi katika nyumba hiyo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 huku akiitumia katika kuandaa kipindi chake maarufu cha Keeping Up With the Kardashians.

                    

Nyumba ya Kim inayopigwa mnada

Mume wa pili wa Kim, Kris Humphries ambaye alikuwa mchezaji wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), naye aliishi katika nyumba hiyo kabla ya wawili hao kuachana kwa talaka baada ya kuwa ndani ya ndoa kwa siku 73.

Baada ya kukamilisha talaka yake na Humphries mwaka 2013, Kim aliiweka nyumba hiyo sokoni ili kwenda kuishi na mume wake wa tatu Kanye West ambaye alifunga naye ndoa mwaka uliofuatia.

Kim alikuwa mke wa Kanye tangu Mei 2014 hadi Novemba 2022 walipoachana kwa talaka, huku wakiwa wamejaliwa watoto wanne, North (2013) na Saint (2015), huku Chicago (2018) na Psalm (2019) wakizaliwa kwa njia mbadala.

Nyumba hiyo yenye vyumba vitano na mabafu sita hapo awali iliwekwa sokoni kwa Dola5.7 milioni. Madalali waliopewa kazi hiyo wameiambia People kuwa nyumba hiyo ni mali yenye thamani na hakuna anayeweza kuikataa.

Hatua hiyo inakuja mwaka mmoja baada ya Kim kusema ununuzi wa jumba lake la kifahari huko Malibu, California ilikuwa sehemu nyingine ya kufurahia na kuandika kumbukumbu mpya za maisha baada ya kukamilika kwa talaka yake na Kanye.

Katika kipindi chake, The Kardashians kilichoruka Julai 2023, Kim aliongozana na watoto wake wote pamoja na dada yake, Khloe Kardashian kutembelea nyumba hiyo ambayo aliinunua mnamo Septemba 2022.

“Nilinunua nyumba huko Malibu, hii imekuwa ndoto yangu ya kila siku, ni miongoni mwa vipindi ambavyo nilikuwa siwezi kuamini kuwa nitalifikia lengo ambalo sikuwaza kama kweli litafanikiwa.” alisema Kim katika kipindi chake.

Mrembo huyo ambaye kwao walizaliwa wanne, Kourtney, Kim, Khloe na Rob Kardashian, alianza kung’ara katika ulimwengu wa mitindo mwaka 2003 akiwa mwanamitindo binafsi wa mwimbaji wa RnB, Brandy.

Mwaka 2015 jarida la Time lilimuweka Kim katika orodha ya watu 10 wenye nguvu ya ushawishi duniani. Na 2021 akawa bilionea ambapo hadi kufikia 2024 Forbes wanakadiria utajiri wake kufikia Dola.17 bilioni, utajiri wake umechochewa na kampuni yake ya Skims.