Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndani ya Boksi: Mnalilia Arena tu, kutumbuiza 'laivu' aaah!

Muktasari:

  • Mondi mtu wa misele mingi. Anapita maeneo mengi ya dunia. Anakutana na midude katika mataifa ya wenzake. Anakatika stimu kuona hapa Bongo bado hatuna maujanja hayo. ‘Imejini’ Rwanda wana Arena.

Dar es Salaam. Yes! Arena siyo kwa ajili ya muziki tu. Lakini muziki una nafasi kubwa. Ndiyo maana kelele nyingi ni za wanamuziki kuitaka Arena. Wanaitaka kwa sababu majirani zenu wanazo na wanatamba sana. 

Mondi mtu wa misele mingi. Anapita maeneo mengi ya dunia. Anakutana na midude katika mataifa ya wenzake. Anakatika stimu kuona hapa Bongo bado hatuna maujanja hayo. ‘Imejini’ Rwanda wana Arena.

Rwanda ni kama Singida au Manyara. Ni kanchi kadogo sana. Mpaka sasa bado sijamjua staa yeyote wa muziki kutoka Rwanda. Zaidi ya Wainjilisti wa “Mkono Wake Bwana”. Lakini wana Arena yao sisi wenye wasanii kibao hatuna.

Bongo ni nchi kubwa yenye wasanii wakubwa Afrika Mashariki. Inakuaje tunakosa Arena? Au ndiyo kutimiza ile misemo ya Wahenga, kama ule wa kwenye miti hapana wajenzi? Inakata stimu kinomanoma. 

Rwanda wengi mashabiki wa Mondi. Wengi mashabiki wa Konde. Wengi mashabiki wa Bongo Fleva. Hutuona sisi kama wakubwa. Na wanapaswa kutuiga kila kitu. Wanapomiliki vitu ‘ameizing’ ambavyo hatuna. Inakata.

Sisi tunatakiwa kuwa juu kwa kila kitu. Kwao tuwatamani dada zao tu. Haifai sisi kutamani vitu vya Rwanda kama hiyo Arena. Haiwezekani! Wanyarwanda ndiyo wanatakiwa waje kushangaa kila kitu chetu. 

Hawana wasanii wakali. Hawana miaka mingi toka watulie kisiasa. Na hawana lugha tamu ya kuimbia. Ujue ni Kiingereza, Kiswahili, Kilingala na Kizulu. Ndiyo lugha zinazovutia kwenye muziki. Siyo Kinyarwanda.

Kuna lugha mtu akiimba ni kama vile anakufokea. Au ni kama vile anaagua majini. Sasa watu ambao hata utajiri wa lugha tamu ni mgogoro. Inakuaje wakae mbele yetu? Arena inahitajika sana na tumechelewa. 

Arena ni eneo ambalo linajengwa kwa shughuli mbalimbali. Achana na hizo mishe za muziki. Michezo na matukio mengi yatafanyika hapo. Kuna ‘ishu” nyingi hufanyika Kwa Mkapa badala ya kwenye Arena. Matumizi ya ovyo.

Arena ni eneo la matukio kibao ikiwa ni pamoja na muziki na burudani zote. Kukosekana kwa Arena, ndiyo maana kina Mwamposa wanafanyia pale kwa Mkapa Injili zao. Ni matumizi mabaya ya uwanja wetu wa soka.

Kukosekana kwa Arena, ndiyo maana kina Mondi huzipeleka shoo pale Kwa Mkapa. Kukosekana kwa Arena, ndiyo maana matukio makubwa hufanywa katika maeneo ya wazi. Ni uharibu tu wa mazingira. Arena ni lazima.

Lakini wanaopigania Arena, wakoje? Wanaweza kuitumia? Hata wakiweza je ni kwa viwango vya Arena? Au wao wanalilia Arena ili mradi wawe sawa na wenzao? Yaani kwamba iwepo tu? Tujipime katika hili.

Maana wanaolilia sana hawana hivyo viwango vya Arena. Wanalilia akili na mitazamo yao ikiwa ni ya Diamond Jubilee. Wanataka Arena ila kazi zao ni za Jamhuri Stadium, kama siyo Nang’wanda Sijaona. Daraja tofauti.

Kazi zetu ziende sawa na tunacholilia. Siyo tunaletewa Arena, inakuwa eneo la mbu na popo. Maana miye sioni kazi za Kiarena nchi hii. Siyo kwa muziki siyo kwa filamu. Wengi hawana akili ya dunia ya Arena inavyotaka. Wako nyuma.
Unataka Arena, lakini huna nidhamu ya kazi. Huwezi ‘kumeneji’ muda wa shoo. Huna 

pumzi ya kuimba kwa saa kadhaa jukwaani. Kila baada ya mstari mmoja wewe unaleta mambo yako ya : “Tuendelee ama tusiendelee”?

Kila msanii akienda jukwaani utasikia “Kushoto, kulia, mikono juuuu, piga keleleeee... tuimbe kwa pamojaaa...” Na makele ya namna hiyo. Mnapaswa kubadili fikra kwanza kabla ya kuwaza miundombinu bora zaidi.

Toka uwanja wa Mkapa ujengwe. Ni hivi karibuni tu umetumika vizuri. Kwa timu zetu kufika mbali kimataifa. Na hata timu ya taifa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali. Lakini muda mrefu haukutendewa haki. 

Lakini pamoja na hilo, mashabiki wa soka wameendelea na ushamba wao. Juzi kati tumeshuhudia waharibifu wakivunja viti. Msalani kuchafu siyo kwa sababu ya kutosafishwa, bali kutokana na matumizi mabaya.

Ustaarabu ni ziro. Je, hiyo Arena yetu tumejiandaa nayo? Sio kujiandaa kwa kuishangaa, bali kwa kuitumia vyema. Akili za mashabiki wa soka na muziki ni walewale. Sasa tuwe tayari kubadili akili zetu kwanza kabla ya vitu.

Mapokeo ya vitu vipya yawe sawa na mabadiliko ya mitazamo yetu. Yes, ni vizuri kupigania ujenzi wa Arena kwa sababu ina faida zaidi kwa sanaa. Ila kuomba Arena, wakati kuimba ‘laivu’ hatuwezi ni undezi. Tenda undezi sana.
Mnapigia kelele Arena kuimba ‘laivu’ aaaah!