TMA yatangaza mvua kubwa siku tatu mfululizo

Muktasari:
- Mvua kubwa zinatarajia kunyesha mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuanzia leo Alhamisi. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewakata wananchi kuchukua tahadhari.
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza angalizo la mvua kubwa kwa siku tatu mfululizo katika maeneo mbalimbali nchini, kuanzia leo Alhamisi, Machi 27, 2025.
Taarifa ya TMA imesema mvua hizo kubwa zinaweza kusababisha baadhi ya makazi kuzungukwa na maji. Kwa leo Alhamisi Machi 27, mikoa iliyotajwa kuwa na mvua ni Mara, Kagera, Geita, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Kigoma, Tabora na Katavi.
Kesho Ijumaa, mikoa inayotarajiwa ku[pata mvua hizo ni Mara, Geita, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Mikoa mingine ni Singida, Dodoma, Tabora, Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Taarifa hiyo ya TMA, imesema mvua hizo kwa Jumamosi Machi 29, 2025, zinatarajiwa kunyesha Mara, Kagera, Geita, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma na Tabora.