Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Michezo ya Harmonize, Kajala hata Ne-Yo na Crystal waliicheza

Muktasari:

  • Hayo yote yalijiri katika sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Amarah ambaye ni mtoto wa binti wa Kajala, Paula

Dar es Salaam. Baada ya kuachana kwa maneno makali kwenye mitandao ya kijamii hatimaye Kajala na Harmonize, wameuacha umma kwenye mshangao baada ya kuonekana katika ukaribu unaodhaniwa kuwa wamrudiana.

Hayo yote yalijiri katika sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Amarah ambaye ni mtoto wa binti wa Kajala, Paula.

Ukaribu wa wawili hao unagongelea msumari msemo usemao "mapenzi hayashauriki". Utakumbuka wamekuwa na historia ya kurudiana na kuachana kama ilivyo kwa penzi la nyota kutoka nchini Marekani Ne-yo, na aliyekuwa mkewe Crystal Smith.

Mapenzi ya Kajala na Harmonize yalifahamika rasmi Februari 2021. Yakavunjika baada ya kusambaa kwa picha za utupu ambazo ilielezwa Harmonize alimtumia mtoto wa mpenzi wake huyo.

Hata hivyo, licha ya kuachana kwa kishindo na maneno, wawili hao walisameheana na  Juni 25, 2022 walichumbiana ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu walipotengana.  

Ikumbukwe walipoachana  Harmonize alimfungulia mashtaka Kajala na binti yake Paula akiwatuhumu kuvujisha picha zake za utupu.

Aidha licha ya kurudiana kwao penzi hilo lilivunjika tena miaka miwili iliyopita na kila mmoja akafuata njia yake. Lakini sasa wameibua tena mjadala kutokana na mabusu waliyopigana kwenye sherehe ya mjukuu wa Kajala.

Hili la wawili hawa unaweza kulifananisha na lile la Ne-yo, na aliyekuwa mkewe Crystal Smith ambaye walifunga ndoa ya pili baada ya ndoa yao iliyodumu miaka minne kuvunjika kwa talaka mwaka 2020.

Wawili hao ambao walifunga ndoa ya kwanza mwaka 2016 nao wamekuwa na mchezo kama wa Kajala na Harmonize  wa kuachana na kurudiana. Hata baada ya kurudiana kwa kula kiapo cha ndoa ya pili mwaka 2021 waliachana tena 2022.

Taarifa ya ndoa yao kuvunjika tena ilitolewa na Crystal Smith mapema Julai 31, 2022 akitangaza rasmi kuachana na mumewe, ambaye wamebarikiwa kupata watoto watatu.

Alisema , “Miaka 8 ya uwongo na udanganyifu. Miaka 8 bila kujua kugawana maisha yangu na mume wangu, na wanawake wengi wanaouza miili yao kwake bila ulinzi. Nimeumia moyoni na kuchukizwa ni jambo lisiloeleweka.”

“Kuniuliza nibaki na kukubali ni wendawazimu kabisa, sitadanganya tena umma au kujifanya kuwa hii sio kitu. Ninachagua mimi, ninachagua furaha yangu, afya na heshima yangu. Nilipata watoto 3 wazuri kutokana na hili lakini hakuna kingine bali maumivu ya moyo,” ameandika Crystal.