Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kusah: Sijakimbia gharama, kuzindua Ep kijijini

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwananchi , Kusah amesema sababu iliyopelekea kufanya hivyo  ni kubadilisha mtazamo wa vijana waliokata tamaa.

Dar es Salaam. Waswahili husema "mkataa kwao mtumwa". Hivyo basi mwanamuziki wa Bongo Fleva  Kusah ameukataa utumwa baada kwenda kuzindua EP yake  ‘Bumbuli Boy’ nyumbani kwao Bumbuli mkoani Tanga.

Akizungumza na Mwananchi , Kusah amesema sababu iliyopelekea kufanya hivyo  ni kubadilisha mtazamo wa vijana waliokata tamaa.

"Mimi nimeamua kuifanya hii kitu local kabisa na iwe kijijini kwetu ili kuwapata watu wote, hata ambao nilikuwa nikiwamisi. Nimetokea, nimesoma Bumbuli najua changamoto za vijana wengi.

“Najua vitu vinavyowakumba watu wengi huku, sio tu nimekuja kufanya Ep ya Bumbuli Boy. Nimekuja kuongea na vijana kubadilisha mtazamo wao kwa sababu sisi ni kioo cha jamii muda mwingine tunavyoongea inakuwa rahisi wao kuwafikia,”amesema

Kusah amesema kuna utofauti mkubwa kati ya vijana wa kipindi chake na vijana wa sasa. Hivyo Bumbuli Boy ni kwaajili ya kuwapa hamasa na kurudi kwenye mstari. "Zamani wakati mimi nasoma tulikuwa tukitoka shuleni tunaenda mpirani au umechukua boda yako kwa hiyo tulikuwa bize sana. Lakini sasa hivi wanakunywa pombe, wala hawana watu wa kuwahamasisha," amesema Kusah.

Hata hivyo amesema kuzindulia EP yake kijijini kwao imekuwa na gharama zaidi ya angefanyia mjini.

"Kufanyia kijijini imekuwa na gharama kuliko tungefanyia mjini. Kwa sababu mimi pekeyangu nimesafiri na watu zaidi ya 17 hawa watu wote kila mtu anafanya kazi na lazima alipwe. Tumekaa huku zaidi ya siku kumi.

“Lazima maisha yaendelee kwa sababu wanafamilia. Pia kuchukua Production nzima ya kushutia video kukaa nayo siku 10 ni kitu kikubwa sana ndiyo maana vitu vimekuwa vya viwango kwa hiyo gharama yake imesimama," amesema Kusah.

Ep ya Bumbuli Boy ilitoka Septemba 25, 2025, ikiwa na jumla ya nyimbo sita ambazo ni Ananipenda, Matamu, Feelings ft Khaligraph Jones, Umekonda ft Yammi, Kwa Heshima, Pombe ft Chino Kidd, Loui.

Utakumbuka kabla  ya Bumbuli Boy, Kusah aliwahi kuachia Romantic mwaka 2022, ikiwa na jumla ya nyimbo tano ambazo ni On Fire, Utaniua, Magical, Shemeji Yenu, Jimwage.