Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kolabo mbili zinazosubiriwa kwa hamu Bongo

Muktasari:

  • Pamoja na wimbi kubwa la kolabo zilizowahi kufanyika. Bado kuna nyimbo mbili ambazo mashabiki na wadau wa muziki wamekuwa wakizisubiri kwa hamu kubwa bila kujua kama ipo siku zitafanyika

Dar es Salaam. Sekta ya muziki wa Bongo Fleva imeendelea kukua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. Huku wasanii wakubwa wakishirikiana katika nyimbo mbalimbali zinazotikisa ndani na nje ya Bongo.

Pamoja na wimbi kubwa la kolabo zilizowahi kufanyika. Bado kuna nyimbo mbili ambazo mashabiki na wadau wa muziki wamekuwa wakizisubiri kwa hamu kubwa bila kujua kama ipo siku zitafanyika.

Kolabo hizo ni kati ya Diamond Platnumz na Alikiba, pamoja na ile ya Diamond Platnumz na Marioo.

Kwa upande wa Marioo, msanii huyo ameendelea kujijengea nafasi yake kama mmoja wa wanamuziki wenye ushawishi mkubwa katika kizazi cha sasa.

Katika safari yake ya muziki, tayari amefanya kazi na wasanii makubwa kama Alikiba, Harmonize, Rayvanny, Jux, Aslay, Darassa, Jay Melody na wengine wengi.

Licha ya mafanikio hayo, jina la Diamond bado halijaonekana katika orodha ya wasanii aliowahi kushirikiana nao, jambo linaloendelea kuibua kuwapa hamu zaidi mashabiki.

Mbali na Marioo yupo Alikiba ambaye tayari amefanya kazi na wasanii mbalimbali wakubwa akiwemo Harmonize, Rayvanny, Mbosso, Marioo, Aslay, Darassa na mkongwe Dully Sykes. 

Lakini pamoja na historia hiyo ndefu ya ushirikiano, bado hajawahi kuachia wimbo rasmi akiwa na Diamond.

Ndivyo ilivyo kwa Mondi katika orodha yake ya kolabo zake, majina kama Alikiba, Marioo na Aslay bado hayajaonekana. Kolabo ya Diamond na Alikiba imekuwa kama ndoto kwa mashabiki. 

Ushindani wa kimuziki kati ya mastaa hao wawili umekuwa moja ya simulizi kubwa zaidi katika historia ya muziki wa Tanzania. Hali inayowafanya wengi kuamini wimbo wao pamoja unaweza kuvunja rekodi nyingi za usikilizaji na kuteka hisia za mashabiki Afrika Mashariki na kwingineko.

Kwa upande wa Marioo na Diamond, wadau wengi wanaamini kuwa mchanganyiko wa vipaji vyao unaweza kuzaa hit nyingine kubwa kutokana na uwezo wao wa kutengeneza nyimbo za mapenzi na zenye mvuto mkubwa.

Licha ya matarajio hayo, hakuna upande ambao hadi sasa umeweka wazi kama kuna mpango wa kufanya kazi pamoja. Kila mmoja ameendelea na ratiba zake za muziki huku mashabiki wakibaki na hamu ya kuona siku moja wakikutana studio na kuachia kazi inayoweza kuandika historia.

Swali linalobaki, je ipo siku mashabiki wataishuhudia kolabo ya Diamond Platnumz na Alikiba au Marioo?