Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Afrobeats, Bill Gates atamani kuwa Mnigeria

Muktasari:

  • Wakati binti yangu aliposikia kwamba nitatembelea Nigeria akasema una bahati sana baba kwa sababu utaonana na Burna Boy na Rema, kwa hivyo ilinibidi kuwatafuta kwa sababu nina shauku sana. 

Marekani. Mmiliki wa kampuni wa Microsoft na bilionea kutoka Marekani Bill Gates amefunguka kuwa anatamani kuwa Mnigeria kufuatiwa na kuzikubali ngoma za Afrobeats.

“Kama nisingekuwa Mmarekani, labda ningekuwa Mnigeria. Wanigeria ni wabunifu sana, afrobeats ni maarufu kila mahali na mimi mwenyewe ni shabiki wake. 

Wakati binti yangu aliposikia kwamba nitatembelea Nigeria akasema una bahati sana baba kwa sababu utaonana na Burna Boy na Rema, kwa hivyo ilinibidi kuwatafuta kwa sababu nina shauku sana. 

"Lakini nakumbuka mara ya mwisho nilipokwenda Nigeria, nilipata kuwaona Davido na Wizkid wakitumbuiza na nilivutiwa sana. Nilipotembelea Nigeria, watoto wangu waliniambia nimekuja nyumbani kwa African Entertainment.

Nadhani ni kweli, Nigeria ni pinacle ya African Entertainment au ningesema kama wanavyopenda kuiita, 'The Giants Of Africa,” alisema Bill Gate kwenye moja ya mahojiano yake ya hivi karibuni.

Hata hivyo, aliweka wazi kuwa tamanio lake kwa sasa ni kuona Burna Boy, Davido, Wizkid na Rema wakitumbuiza kwenye steji moja huku akiahidi kulipa kiasi chochote cha fedha.