Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Johari: Kila msanii na enzi zake, mashabiki wake

Muktasari:

  • Maendeleo ya teknolojia yalivyozidi kushika kasi CD zilitikisha katika ‘deki’ za watu huku filamu nyingi zilizooneshwa hazikukosa sura ya Kanumba, Johari na Ray.

Dar es Salaam. Runinga nyingi kuanzia  mwaka 2005 hadi 2012 zilipambwa na michezo ya maigizo huku wasanii wake wengi wakitokea katika vikundi kama kile cha Kaole.

Maendeleo ya teknolojia yalivyozidi kushika kasi CD zilitikisha katika ‘deki’ za watu huku filamu nyingi zilizooneshwa hazikukosa sura ya Kanumba, Johari na Ray.

Ukweli ni kwamba maendeleo hayo yanaendelea kukua na kuibadili sekta ya filamu nchini. Kwa sasa si CD tena bali ni tamthilia mpya kila kukicha.

                       

Uwepo wa tamthilia hizo katika visimbuzi mbalimbali umeendelea kuwainua baadhi ya waigizaji na waandaaji akiwemo Blandina Chaula ‘Johari’ ambaye mwaka 2024 umegeuka kumbukumbu kwake.

Mwigizaji huyu Desemba 1,2024, kupitia tamthilia ya Yolanda nchini Afrika Kusini alifanikiwa kunyakua tuzo mbili za ZIKOMO katika kipengele cha Msanii Bora na Tamthilia Bora. Hata hivyo, usiku wa kuamkia Septemba 15,2024 nchini Nigeria alinyakua tena tuzo ya MVAA kama Mwigizaji Bora Afrika.

Kutokana na maneno ya baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii kutoamini ushindi wake mwigizaji huyo anasema kushinda tuzo ni haki yake. 


                      

“Katika maisha siyo wote wanaongea wengine wanapiga kelele mimi nawachukulia kama wanapiga kelele, kwa hiyo mtu mmoja hawezi kukosoa jopo la watu 20 waliokaa tena watu wa nchi mbalimbali.

“Mtu akisema sistahili basi atakuwa anastahili yeye lakini mimi ninayefanya kazi yangu naona kuzipata ni haki yangu kwa kazi ambazo nazifanya,”anasema Johari.

Anasema ili Tuzo za Filamu nchini zifanye vizuri zinatakiwa kutolewa bila upendeleo. 

“Tanzania tusiangaliane usoni tupeane kutokana na kazi ambayo mtu anaifanya, lakini tuzo nyingi za Tanzania tumekuwa tukipeana machoni kwa kuangalia huyu ni fulani.

“Tusipange matokeo tutoe tuzo kutokana na uhalisia wa kazi ya mtu na watu wanaostahili naweza kusema tujipange sana katika tuzo za nyumbani,”anasema.

Johari ambaye kwa sasa anafanya vizuri pia kama mzalishaji wa filamu nchini anasema uyumbaji wa soko la filamu moja moja ndiyo kuliwapeleka kwenye utengenezaji wa tamthilia. 

“Tupo kote lakini soko la ‘single movie’ lilikuwa limeyumba kidogo tukaamua tuhamie kwenye upande wa series.
“TV zipo nyingi ambazo zinaonesha kwa hiyo soko ndiyo linatufanya hivyo lakini pia hatujaacha bado tunatengeneza na usipoangalia kwenye TV unaweza ukaingia YouTube,” anasema. 


Haamini Kanumba kufa na Bongo Movie

Tangu kitokee kifo cha aliyekuwa mwigizaji wa Bongo Movie mwaka 2012,  marehemu Steven Kanumba, kumekuwa na mitazamo inayodai kuwa alifariki na Bongo Movie.

“Maneno kuhusu Kanumba tangu afariki hayana ukweli wowote alikuwa  na mashabiki wake na anacheza kwenye nafasi yake na kila mtu ana shabiki wake. 

“Mimi naona kama imani potofu na kupotosha katika tasnia hata tufe sisi wote vizazi vitaendeleza, mtu akisema tasnia imekufa kwa sababu ya mtu mimi nakataa lakini tasnia ipo na itakuwepo,”anasema.


                         

Anasema kinachodumaza Bongo Movie ni baadhi ya waongozaji kuwapa uhusika watu wasiopenda sanaa na wenye majina makubwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunadumaza tasnia tunatakiwa kuweka wasanii wanaopenda sanaa, mtu akijua  na akapenda sanaa anaweza akavumilia vitu vingi sana tunatakiwa tuweke wasanii. 

“Maproducer tusiwe wachoyo tusiweke watu ambao hawana moyo na sanaa tuchukue wasanii wachanga tuwafundishe waweze kujua sanaa tuweze kupata wasanii wazuri hata ukiangalia kwenye series ya Yolanda wasanii wachanga wengi,”anasema. 

Anasema ili tasnia ya filamu nchini ifanye vizuri ushirikiano na umoja unahitajika.

“Wenzetu wanaushirikiano katika kazi zao unakuta mtu anajua kwamba hiki nachofanya naungana na wenzengu hata sisi tukitaka tasnia yetu ifike mbali lazima tufanye ushirikiano na tuwe na umoja,” anasema Johari.