Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya utajiri wa Diamond, Vunjabei amuonya Mwijaku

Muktasari:

  • Katika ujumbe huo kwenye mtandao wa Instagram, Fred Vunjabei ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya Vunjabei Group Limited na Rais wa Too Much Money Company amesisitiza umuhimu wa kuheshimu bidhaa za wateja na uhusiano na watu wengine

Dar es Salaam. Mfanyabiashara, Fred Ngajiro maarufu ‘Vunjabei’ ametoa onyo kwa mtangazaji, Mwemba Burton maarufu ‘Mwijaku’ kupitia ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii.

Hayo yanajiri baada ya hivi karibuni msanii Naseeb Abdul maarufu kama ‘Diamond Platinumz’ kutangaza ndoto yake ya kuwa tajiri namba moja duniani ndipo Mwijaku akaibuka na kupinga kauli ya Diamond kwa kusema kuwa hajafikia hata asilimia 40 za utajiri wa mfanyabiashara Fred Vunjabei, hivyo bado ana safari ndefu huku akiahidi kuwaandalia mdahalo wa kutaja mali zao.

Katika ujumbe huo kwenye mtandao wa Instagram, Fred Vunjabei ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Vunjabei Group Limited na Rais wa Too Much Money Company amesisitiza umuhimu wa kuheshimu bidhaa za wateja na uhusiano na watu wengine.

"Ni kweli tunahitaji huduma zenu kwenye biashara zetu, lakini ifike point mziheshimu brands za wateja wenu na uhusiano wao na watu wengine, kuna maisha baada ya mitandao ya kijamii."

Vunjabei amesema kuwa ameshamwonya Mwijaku mara nyingi na hata kufungua mashtaka dhidi yake, lakini mambo yaliisha baada ya Mwijaku kutuma watu kumwomba wayamalize.

Aidha, Vunjabei amemsisitiza Mwijaku kuacha tabia hiyo; "Nimeshakuonya mara nyingi, nilikufungulia mpaka mashtaka ukatuma watu yakaisha, nasema mara ya mwisho nakuomba koma mara moja kunitaja au kutaja kampuni yetu vinjabei kwenye mambo yako," ameandika Vunjabei.

Hata hivyo, Mwijaku alijibu ujumbe huo kwenye chapisho hilo la Vunjabei aliloliweka Instagram kwa kuandika: "Kwa hiyo ni kweli madeni ya benki yanakukimbiza mjini tajiri @fred_vunjabei"