Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afande Sele alivyowakalisha Mwana FA, Profesa Jay

Muktasari:

  • Moja ya tukio kubwa ambalo limeacha alama kwenye muziki wa Bongo Fleva ni pamoja na shindano la kumsaka Mfalme wa Rhymes lililofanyika mwaka 2004 likiwa chini ya uratibu wa  Eric Shigongo ambaye kwa sasa ni mbunge wa Buchosa.

Dar es Salaam. Ikiwa leo ni Alhamisi ya tarehe 6, Machi 2025 siku ambayo watu wengi huitumia kukumbuka baadhi ya matukio na mambo yaliyotokea miaka ya nyuma. Moja ya tukio kubwa ambalo limeacha alama kwenye muziki wa Bongo Fleva ni pamoja na shindano la kumsaka Mfalme wa Rhymes lililofanyika mwaka 2004 likiwa chini ya uratibu wa  Eric Shigongo ambaye kwa sasa ni mbunge wa Buchosa.

Shindano hilo lililoibua msisimko mkubwa kutokana na kubeba majina ya wasanii wakubwa na pendwa zaidi kipindi hicho hali iliyopelekea ugumu katika maamuzi.

Katika kinyang'anyiro hicho wasanii walikuwa mahiri kwenye uandishi wa mada za kuelimisha na kuburudisha lakini baada ya mchujo kupita yakapatikana majina 10 ili kumpata mmoja ambaye angevikwa taji la Ufalme wa Rhymes na kuondoka na zawadi ya gari. 

Shindano liliwakutanisha kumi Bora iliyoshiba majina ya wasanii waliokuwa na ngoma Hit wakati huo ambao ni Jay Moe 'kama unataka demu', Afande Sele 'Darubini Kali', Prof J 'Zali La Mentali', Inspector Haroun 'Bye Bye', Solo Thang 'Mtazamo', Madee 'Kazi yake Mola', Mwana FA 'Unanitega', Mandojo na Domokaya 'Nikupe Nini', Soggy Dogy 'Kulwa na Doto' na Dully Sykes, ambaye alijitoa siku chache kabla ya shindano.

Usiku wa Ijumaa Juni, 27, 2004 ukumbi ulifurika wadau na mashabiki kutoka sehemu mbalimbali na baada ya majaji kufanya mchakato washindani waliyobaki ni Afande Sele na Inspector Haroun wengine walikatwa tukio lililoibua mshangao mkubwa huku wengi wakihoji mbona hatumuoni Prof Jay na wengine.

Afande Sele akatangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo na kutawazwa kuwa mfalme wa Rhymes mwaka 2004 mshindi wa pili alikuwa Inspector Haroun na watatu walikuwa kina Mandojo na Domokaya (kundi).

Ushindi wa Afande Sele uliandamwa na ukosoaji mkubwa huku wasanii kadhaa wakidai kuwa Afande alipendelewa na ilipangwa ashinde.

Haikupita muda Solo Thang aliandika wimbo 'Kilio Changu' akimshirikisha Q Chief akipinga kile kinachoitwa kupanga mshindi, namnukuu "Wengine wananirubuni eti nashindania gari, kumbe washapanga wampe nani toka awali, sitarudia kosa hata zawadi waweke meli, wanipe ghorofa mbili wanikabidhi na sheli" 

Solo Thang hakuishia hapo, katika wimbo wa 'Traveller' anasikika tena akisema "Mi siyo mfalme njozi mi siyo mgambo Sele"

Rapa Fid Q naye katika ngoma yake ya 'Mwanza Mwanza' aliendelea kuthibitisha kutokukubalika kwa ufalme wa Afande, namnukuu "Mfalme wa Rhymes ambaye Soggy Doggy hamtaki, anamwita Kobe hawezi mzidi mbio farasi"
Msanii Madee naye alienda mbali na kudai hajawai ona mfalme ana nywele chafu.

Sasa ni takribani miaka 21, imepita tangu Afande Sele atangazwe kuwa Mfalme wa Rhymes na hajapata mrithi wake, mwaka 2005 shindano halikufanyika baada ya washiriki kudai maslahi zaidi huku wengine wakipinga kwa kuhofia kupangwa mshindi ambaye ilisemekana alitakiwa kuwa Fid Q, ambaye alishajinadi kuwa ni mfalme atakayefuatia baada ya Selemani Msindi.

Hata hivyo, kupitia mahojiano aliyofanya Afande Sele kwenye kipindi cha Ladha 3600 cha EFM alidai kuwa kama shindano hilo likirudi tena, wapo rapa wanaostahili kuvikwa taji lake ambao ni pamoja na Darassa, Stamina, Roma na wengine.

“Naumizwa kuona kwamba Mfalme wa Rhymes ni tukio ambalo halifanyiki tena wakati watu wanataka lifanyike, kipindi fulani tulikuwa na uhaba wa rappers wazuri lakini kipindi hiki kuna rappers wazuri kuanzia akina Darassa, Roma, Stamina, Kala na wengine wengi,” alisema Afande Sele.