Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Ramani ya kumuua Steve Nyerere ilichorwa hivi'

Muktasari:

  • Licha ya kuigiza sauti za viongozi, amekuwa akifanya shughuli nyingine kama vile muziki, maigizo, vichekesho harakati na hata siasa

Jina lake wengi walianza kulifahamu kutokana na kuigiza sauti za viongozi mbalimbali huku ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere na mwanasiasa Augustine Mrema, ikiwa imekubalika zaidi kwa mashabiki wake hadi kumpatia jina la Steve Nyerere, licha ya kuwa jina halisi ni Steve Megele.

Licha ya kuigiza sauti za viongozi, amekuwa akifanya shughuli nyingine kama vile muziki, maigizo, vichekesho harakati na hata siasa.

Steve amefanya mahojiano na Mwananchi na kulieleza kuwa alianza harakati za kujitafuta mwaka 1997, akiwa shule, kwa kuigiza sauti za viongozi ambapo alikuwa akisifiwa kuwa anafanya vizuri kila alipokuwa akizungumza.

Alivyoanza kujitafuta

“Nimeanza kujitafuta mwaka 1997, mimi nimezaliwa Kinondoni Bwawani, nimesoma Kinondoni School baada ya hapo, tukahamia Mwanza nikasoma shule inaitwa Buzuruga Nyakato, tuliondoka na familia na kwenda Tabora, hapo ndiyo nikaanza kuigiza sauti za viongozi wote.” amesema Steve.

Anasema baada ya kumaliza darasa la saba alirudi tena Biafra, Dar es Salaam kuanza kidato cha kwanza, huku wakati huo akiwa anakwenda kwenye kikundi cha Uigizaji Kaole kwa ajili ya kuendeleza kipaji chake.

 “Nilikuwa nakwenda Kaole nakutana na marehemu Max, Steven Kanumba, Vincent Kigosi (Rey), Mahsin Awadh (Dk Cheni), Nora, Nina, Nana nawaigizia sauti, sasa Saidi Banda (Max) akawa ananichukua akiwa Mc, muda wa kula mimi nakuwa Nyerere naigiza sauti ya baba wa Taifa ukumbini watu wanafurahi sana.

"Wakati huo natoka Kinondoni naenda Magomeni natembea hadi lango la jiji, nikajiongeza nikawa naenda Twanga Pepeta nabeba spika za Twanga, nafagia hakuna aliyekuwa ananijua hakukuwa na ubaya nilikuwa hadi napelekwa mikoani kubeba spika, lakini silipwi chochote.” Anasema Steve.

Anasema safari yake ya kuigiza iliota mizizi zaidi baada ya marehemu Kanumba kumpa sini ya kumuelekeza nyumbani kwao kwenye tamthilia iliyoitwa ‘Kaole’, ndipo watu wakampokea kwenye uigizaji na kuendelea kutikisa hadi sasa.

Hadi sasa Steve amefanikiwa kucheza filamu sita, huku akiwa amepita kwenye kikundi kimoja ‘Kaole’, na kazi nyingine akiwa anafanya mwenyewe kwa kujitegemea.

'Steve kutaka kuuawa kwa kuwekewa sumu'

Licha ya kuwa wapo wanaompenda kutokana na vipaji vyake vya kuburudisha Steve amedai kuwa anakumbana na changamoto ya kuchukiwa, huku akisimulia alivyonusurika kifo mwaka 2015, baada ya kuwekewa sumu kwenye chakula.

“Miaka ya nyuma nilivyomaliza kampeni ya aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, unajua kwenye kampeni kila mtu anamtafutia mgombea wake nafasi kwa hiyo chuki zinakuwa nyingi, kuna sehemu moja nilikuwa nakula, baada ya muda Jacob Stephen (JB), alivamia chakula changu yeye akasanuka wa kwanza akaanza kutapika mimi nikawaishwa hospitali ya Kairuki nikakaa miezi miwili.” Ameeleza Steve.


                                                   

Ramani ya kumuua Steve Nyerere ilichorwa hivi "nililazwa ICU miezi miwili..."

Anasema sumu aliyowekewa ilienda kuganda kwenye kitovu na kumfanya abadilike mwili na kuwa mweusi, huku akipungua maji mwilini na kutoka haja kubwa na ndogo zikiwa na damu.

“Mzee Bernand Membe, alikuwa anakuja kuniona hospitali akawa anasema nipelekwe Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu lakini kuna dokta hadi leo namshukuru aliomba apewe siku mbili za kunifanyia uchunguzi ndipo ikagundulika sumu imeganda kwenye mafuta chini ya kitovu, nilichomwa sindano za ganzi wakaivuta kwa sindano.”

Anaeleza kuwa hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa kipindi nyuma badala yake aliamua kukaa kimya ili kuwaonesha adui zake kuwa wameshindwa kumuua.

'Ramani ilivyochorwa hadi kuwekewa sumu'

Steve amedai baada ya kutokea tukio hilo mpishi wa eneo hilo alikwenda kumuomba msamaha na kueleza tukio lilivyokuwa.

Amedai kuwa kuna mtu alitumia njia ya uongo kumdanganya mpishi wakati anaandaa chakula, kwa kumwambia kuwa ameagizwa na Steve kuweka kitu kwenye chakula kwa ajili ya kuongeza ladha na hamu ya kula, hivyo mpishi alikubali na kuweka kitu hicho bila ya kujua ilikuwa sumu.

“Mpishi wa eneo lile aliomba msamaha, baada ya kuulizwa na vijana wangu alisema alipelekewa kitu na mtu asiyemfahamu akamwambia kuwa yupo na mimi, hivyo nimemuagiza ampe kitu kile ili aniwekewe kwenye chakula kwa ajili ya kuongeza ‘apataiti’.”

Anadai inaonekana kabla ya kuwekewa sumu kuwa mtu alisoma mazingira ya eneo na alichokuwa ameagiza. Kutokana na tukio hilo Steve anasema hakumfahamu aliyefanya kitendo hicho lakini moja kwa moja aliwaza alifanyiwa hivyo kwa sababu ya mambo ya kisiasa kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye kampeni.

 Licha ya kutokea kwa tukio hilo Steve amedai hakuona umuhimu wa kufungua kesi polisi, kwani alikuwa tayari amelazwa kwa muda wa miezi miwili. Hivyo aliamua kusali , kumuachia Mungu na kusamehe.

Aidha Steve amedai kwa upande wa JB ambaye naye alikula hicho chenye sumu alifikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu na kisha akarudi nyumbani.

“JB alikuwa shwari si unajua mwenzangu ana mafuta mengi alifikishwa hospitali akatoka na akaendelea na maisha yake”. Amesema Steve 


Big G ilivyojenga ukaribu wake na Rais mstaafu Jakaya Kikwete

Anasema katika harakati za kupambana kwenye maisha, akiwa mdogo alikuwa akifanya biashara ya kuuza Big G, nje ya Shoppers Plaza Msasani, alikutana na Kikwete na kumfanya awe mteja wake wa Big G na hapo ndipo walianza kufahamiana.

                      

“Nilikutana na Kikwete akiwa Waziri wa Mambo ya Nje, mimi nikiwa nauza Big G, kipindi hicho nilikuwa machachari, nikiona mtu ambaye nimemuona kwenye Tv nashangilia ilikuwa lazima nimfuate, nikamfuata Jakaya nikamwambia anunue Big G akawa ananiungisha. Kitu kimoja ambacho vijana wengi hawajui ni kwamba urafiki hautengenezwi kwa vyeo bali kwa milima na mabonge na hadi leo ni rafiki yangu tukikutana tunaogea na kutaniana.”amesema Steve

Steve kupiga pesa kwa jina la Ally Choki

Anasema miaka ya nyumba aliwahi kwende Kilwa na kujifanya yeye ni Ally Choki kwa ajili ya kupata pesa.
“Nakumbuka tulienda Kilwa Masoko na Kilwa Kivinje kipindi hicho gazeti linafika baada ya wiki moja wakati huo Ally Choki anatamba kweli, tukatoka mimi Kingwendu, Kipemba na mbunge mmoja marehemu sasa hivi alikuwa anaitwa Omary Chubi, mbunge wa Kilwa Masoko akatangaza kwa wananchi kuwa Choki anakuja.

"Kwenye mlango wa ukumbi alikaa mbunge mwenyewe akikusanya mzigo, mimi nikavaa kofia hadi usoni Kingwendu akajifanya Husein Jumbe nilichokuwa nazingatia wenyewe wakipiga bendi mimi naimba kama Choki”. ameeleza Steve


Miaka mitatu ya Rais Samia madarakani

Ikiwa inaelekea miaka mitatu ya Rais Samia tangu aingie madarakani Steve Nyerere amesema imekuwa ni miaka mitatu ya Watanzania kufurahi.

   

                      

                  

“Miaka mitatu ya mama imekuwa ya kufurahi kwa Watanzania, upande wa michezo tumeona wanasarakasi wanapata tuzo hadi Marekani, tulikuwa hatuna ndoto hiyo lakini tulikuwa tunavipaji. Miaka mitatu timu yetu ya taifa tumeshiriki mpaka Afcon, muziki wa Tanzania umetoboa hadi wasanii wa singei sasa hivi wanapata hela kwenye upande wa filamu, Kenya, Rwanda ikifika jioni wanatazama Jua Kali na Huba, miaka mitatu ya mama sanaa inaheshimika.” Amesema Steve

Kauli ya Steve kwa  Mwana-FA kwenye utendaji

Utakumbuka mwaka 2022, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' alitoa saa 48 kwa Shirikisho la Muziki Tanzania kufanya maamuzi ambayo yatawaridhisha wasanii kuhusu nafasi ya Usemaji wa Shirikisho hilo ambao walimpa Steve Nyerere, jambo ambalo lilisababisha pingamizi kwa wasanii

                     

Hivyo basi, ikiwa imepita miaka miwili tangu kutokea kwa tukio hilo, ambapo kwa sasa Mwana-FA ni Naibu Waziri wa Sanaa, Burudani na Michezo Steve ametoa mtazamo wake juu ya utendaji wake kwa kusema kuwa FA ametoka katika sanaa kwa hiyo anafahamu kwa uzuri yanayowakumba wasanii hivyo hawezi kufanya vitu kama hafahamu yanayosumbua wasanii.

“FA anajua changamoto za muziki wa dansi, bongo muvi, mashairi, na kikubwa zaidi  ndani ya mwaka mmoja tumeona changamoto ndogondogo amezitatua. Kikubwa zaidi ni kugawa asilimia 50 kwa kila sekta, isitokee sehemu ikawa kuna 50 kwa 30 hapo itakuwa changamoto lakini hadi sasa FA anafanya vizuri, ni mteule, Rais hakosei anapoteua." Amesema Steve