Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zanzibar yataja faida baada ya kubinafsisha huduma hospitali za umma

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh akijibu maswali ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika kiako cha 30 Baraza hilo Chukwani Zanzibar.

Muktasari:

  • SMZ imesema baada ya ubinafsishaji madaktari bingwa sita wameongezeka.

Unguja. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema baada ya kubinafsisha baadhi ya huduma katika hospitali zake, nyingi zimeanza kuimarika ikiwemo upatanikanaji wa dawa kwa asiliamia 90.

Huduma nyingine zilizoimarika katika hospitali za umma ni usafiri hospitalini, nidhamu ya kazi imeongezeka, chakula cha wagonjwa kinapatikana kwa wakati na ufuaji wa nguo za wagonjwa na uendeshaji wa hospitali umekuwa bora zaidi.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh alipojibu swali la Mwakilishi wa Wingwi, Kombo Mwinyi Shehe aliyetaka kufahamu tangu Serikali iingie mikataba na kampuni binafsi hali ya upatikanaji wa huduma ikoje katika hospitali zake.

Pia alitaka kujua takwimu za vifo vya mama na mtoto zikoje baada ya kuingia mikataba hiyo na kampuni za Lacent, NSK na Seifii.

Kuhusu idadi ya vifo, Naibu Waziri Hafidh amesema tathmini ya ufanisi wa utoaji wa huduma kwa kawaida hufanyika kila mwaka na kwa sasa haijafanyika.

“Hivyo basi, kwa vile mpaka sasa tumetimiza miezi minne tu ya utekelezaji chini ya huduma hii, ripoti kamili ya tathmini ya hali ya vifo vya mama na mtoto itatolewa baada ya kutimiza angalau mwaka mmoja baada ya utekelezaji,” amesema.

Amesema madaktari bingwa walioongezeka kwa baada ya kuwepokampuni hizo, ni sita ambao ni wa magonjwa ya watoto, upasuaji kwa kutumia njia ya matundu, mifupa, huduma za dharura, usingizi na wa pua, masikio na koo.


Kupanua utalii

Wakati huohuo Serikali imetaja mikakati iliyonayo ya kuongeza masoko mapya ya utalii ikiwa ni pamoja na kushirikiana na mashirika makubwa ya utangazaji duniani kutangaza vivutio vipya Zanzibar.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mudrick Ramadhan Soraga ametoa kauli hiyo akijibu swali la mwakilishi wa Mwanakwerekwe, Ameir Abdalla Ameir aliyetaka kufahamu mikakati ya wizara katika kutafuta masoko mapya ya utalii badala ya kuendelea kuzitegemea nchi zilezile zilizozoeleka.

“Wizara imeedelea kushirikiana na ubalozi wa Tanzania nchini China na Korea kuvutia masoko haya mapya yanayokua kwa kasi katika utalii nje ya Bara la Ulaya ili kuwahamasisha watalii kutoka nchi hizo kutembelea Zanzibar,” amesema Soraga.