Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ufaulu kidato cha sita wapanda

Muktasari:

  • Imeelezwa kuwa ufaulu huo wa jumla kitaifa ni asilimia 99.95, ukiwa ni ongezeko la asilimia 0.03 dhidi ya ufaulu mwa mwaka jana uliokuwa asilimia 99.92.

Unguja. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita huku  ufaulu wa jumla ukiwa asilimia 99.95 kwa watahiniwa 126,135 waliofanya mtihani,  sawa na ongezeko la asilimia 0.03 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2024 ambao ulikuwa asilimia 99.92.

Akitangaza matokeo hayo leo Julai 7, 2025 katika ofisi za Necta Zanzibar, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Profesa Said Mohamed, amesema watahiniwa 790 hawakufanya mithani sawa na silimia 0.62.

“Watahiniwa wa shule waliofaulu ni 125, 779 sawa na asilimia 99.95 ya watahiniwa wenye matokeo. Watahiniwa walioshindwa mtihani ni 68 sawa na asilimia 0.05. Mwaka 2024 watahiniwa 103,252 sawa ana asilimia 99.92 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo,” amesema.

Amesema ufaulu wa watahiniwa kwa kuzingatia jinsi unaonesha kuwa wasichana waliofaulu ni 61,953 sawa na asilimia 99.95, huku  wavulana wakiwa 63, 826 sawa na asilimia 99.95.

Amesema takwimu zinaonyesha jumla ya watahiniwa 125, 375 sawa na asilimia 99.62 wamepata ufaulu wa madaraja ya  kwanza hadi la tatu, kati ya hao waliopata daraja la kwanza ni watahiniwa 61, 120 sawa na asilimia 48.57,  daraja la pili ni 49, 385 sawa na asilimia 39.24.

Mwaka 2024 watahiniwa waliopata madaraja ya  kwanza hadi la tatu walikuwa 102, 719 sawa na asilimia 99.40, hivyo kuna ongezeko la ubora wa ufaulu  kwa asilimia 0.22 mwaka huu.