Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SMZ kujenga chuo cha afya Pemba

Waziri wa afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na waandishi wa habari kueleza mafanikio katika  sekta ya afya kwa miaka 60 tangu kuasisiwa kwa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1664.Picha na maelezo

Muktasari:

  • Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kujenga kituo cha afya kisiwani Pemba ili kuongeza idadi ya wataalamu kwenye sekta hiyo.

Unguja. Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, amesema miongoni mwa jitihada inazozifanya kuboresha sekta ya afya ni kuongeza watalaamu wa sekta hiyo kwa njia mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyuo.

Amesema mpango walionao hivi sasa ni kutanua zaidi sekta ya afya kisiwani Pemba kwa kujenga chuo cha kwanza kisiwani humo kitakachotoa watalaamu wa kada hiyo katika shehia ya Kengeja Wilaya ya Mkoani.

Ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Desemba 11, 2023 wakati akizungumza na waanadishi wa habari mjini Unguja, kuelezea mafanikio ya sekta ya afya kwa  miaka 60  tangu Mapinduzi ya  Zanzibar yaliyofanyika mwaka 1964.

Amesema awali Serikali ilipanga kujenga hospitali ya wilaya katika eneo hilo lakini mara baada ya kubadilishwa kwa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani kuwa hospitali ya wilaya wakaona hakuna haja kujengwa kwa taasisi mbili za wilaya kwenye eneo moja.

Waziri Mazrui amesema mkakati wa Serikali kwa sasa ni kulitumia eneo walilopewa na wakazi wa kijiji hicho kujenga chuo cha afya kama kilichopo Unguja wakilenga kuzalisha watalamu wengi zaidi.

‘’Kwa miaka yote hadi sasa Pemba bado hakuna chuo cha afya cha Serikali, hivyo tumeona ni fursa adhimu kwa watu wa Pemba kuwa na chuo chao kitakachowarahishia lakini pia kuwaondolea changamoto kusoma Unguja ambapo hutumia gharama zaidi’’alisema.

Waziri Mazrui amezungumzia kuhusu baadhi ya akinamama wa eneo hilo na maeneo mengine jirani kuacha kujifungulia nyumbani badala yake wakimbilie kwenye vituo vya afya tangu hatua za awali wakati wa ujauzito wao.

Amesema inasikitisha hadi leo kuona baadhi ya akinamama wanakutana  na changamoto wakati wakijifungua huku wakiwa majumbani mwao na wengine wanajifungua wakiwa njiani.

Nao baadhi ya wananchi wa shehia ya Kengeja, wamepongeza uamuzi wa Serikali ana wamesema wanaamini itautekeleza kwa vitendo.

Habib Massoud amesema iwapo mkakati huo wa kujengwa chuo cha afya utafanyika utafungua fursa zaidi kwa kisiwa cha Pemba na kufanya harakati za kila siku kuongezeka katika maeneo mbalimbali.

Amesema chuo huleta watu kutoka maeneo tofauti hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa eneo husika.

Selme Abdalla amesema kujengwa kwa chuo hicho pia kutasaidia kuongeza ari ya vijana kuongeza bidii ya masomo wakiamini ni watu muhimu wenye fursa ya kuendelea kielemu.