Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hivi hapa vikwazo kwa watu wenye usonji

Mwenyekiti wa Jumuiya ya kusaidia watu wenye Tawahudi (Zacso), Munawarah Mahfoudh Haji akizungumza kuhusu kongamano la watu hao litakalofanyika Aprili 8, 2026 Unguja Zanzibar

Muktasari:

  • Watoto na watu wenye usonji wanaweza kuhitaji aina tofauti za msaada kulingana na mahitaji yao binafsi. Hata hivyo, kwa uelewa sahihi, huduma stahiki na mazingira jumuishi, wana uwezo wa kuishi maisha yenye tija na heshima kama watu wengine katika jamii.

Unguja: Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Usonji Aprili 2, imeelezwa kuwa watu wenye hali hiyo wanakabiliwa na changamoto kadhaa, zikiwemo unyanyapaa, vikwazo kwenye elimu, ajira na ushirikishwaji.

Usonji ni hali ya ukuaji wa ubongo inayoathiri uwezo wa mtu katika mawasiliano, uhusiano wa kijamii na tabia. Watoto na watu wenye usonji wanaweza kuhitaji aina tofauti za msaada kulingana na mahitaji yao binafsi.

Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa watu wenye tawahudi wana thamani sawa, wanastahili heshima na haki kamili.

Katika kutambua umuhimu wa kundi hili, limeandaliwa kongamano ambalo linatarajiwa kufanyika Aprili 8, litakalowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya afya, elimu, serikali, mashirika ya kiraia pamoja na jamii kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 3, 2026 kuhusu kongamano hilo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Autism Care and Support Organization (ZACSO), Munawarah Mahfoudh Haji amesema lengo ni kuongeza uelewa wa jamii, kuondoa unyanyapaa na kuhakikisha wanapewa fursa sawa badala ya kuonekana kuwa ni watu wasiofaa.

"Kuhamasisha mtazamo chanya na jumuishi kwa watoto na watu wenye tawahudi, kutoa jukwaa la kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto katika sekta za afya, elimu na jamii," amesema Munawarah.

Pia litaunganisha wataalamu na wadau ili kushirikiana maarifa na mbinu bora za kuwasaidia watu wenye tawahudi na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma za afya, elimu jumuishi na msaada wa kijamii, pamoja na kuhamasisha ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii.

Amesema bado kuna changamoto pia kwa wazazi kuhusu namna ya kuwatambua na kuwahudumia watoto hao, hivyo watahimizwa kutafuta huduma za mapema wanapoona dalili za tawahudi.

Kwa mujibu wa wataalamu, wakati mwingine inachukua muda kwa wazazi kutambua hali hiyo. Utambuzi wake hutofautiana kulingana na mtoto husika, lakini wengi huanza kubainika kati ya miezi 10 hadi 18.

Hivyo, mtazamo wa jamii unategemea uelewa; wapo wanaoshuku au kuwatenga, lakini pia kuna harakati za kukuza ushirikishwaji, kuondoa chuki na kutambua mchango wa watu wenye usonji.

Mmoja wa wazazi mwenye mtoto mwenye usonji, Reuben Juma, amesema walimtambua mtoto wao baada ya kufikisha miezi 12, ndipo walianza kubaini kuwa kuna hali isiyo ya kawaida.

Katika suala la unyanyapaa, anasema linajitokeza mara nyingi kwenye jamii, na wapo wanaoamini kuwa hali hiyo inahusiana na masuala ya kishirikina.

Hata hivyo, anasema changamoto kubwa inayowakabili watu hao ni kutokuwepo kwa vituo vya kutosha vya kuwafanyia mazoezi watoto wa namna hiyo.

"Suala la unyanyapaa ni kubwa. Mtu akishakuwa na mtoto wa namna hiyo, hukutana na mazingira yasiyo ya kawaida katika jamii inayomzunguka. Kikubwa, nadhani elimu bado ni ndogo kwa wananchi, kwa hiyo ni muhimu kukazania sana eneo hili," amesema Juma.

Amesema watathaminiwa pale jamii inapoelimika, kwani kuna upungufu wa ufahamu; wanaweza kukosa kuaminika au kukosa fursa sawa, lakini elimu na ushirikiano vitasaidia kubadilisha mitazamo hiyo.

Licha ya maadhimisho ya Siku ya Usonji Duniani kufanyika kila Aprili 2, Zanzibar wataadhimisha siku hiyo Aprili 8 kwa kufanya kongamano la kutoa elimu.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema, "Autism and Humanity, Every Life Has Value" (Usonji na ubinadamu, kila maisha yana thamani).

Kaulimbiu hii inalenga kusisitiza umuhimu wa kutambua utu, heshima na thamani ya kila mtu mwenye usonji, pamoja na kuhakikisha anapata haki sawa katika nyanja zote za maisha.

//block eskimi