Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima 2,190 mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kunufaika na teknolojia za kisasa

Shughuli za uzalishaji bunifu za zana za kilimo ikiendelea katika Kituo cha Uendelezaji wa Teknolojia Sido Mkoa wa Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Hatua hiyo imekuja baada ya Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (Sido) Mkoa wa Mbeya kuja na mwarobaini wa teknolojia bunifu kuzalisha dhana za kilimo cha kisasa kwa lengo la kuwapunguzia gharama za kuagiza nje ya nchi.

Mbeya. Wakulima zaidi ya 2,190 katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wananufaika na matumizi ya teknolojia za kisasa katika uzalishaji wa mazao ya kimkakati, ikiwemo kuongeza thamani ya malighafi viwandani.

Hatua hiyo imetajwa kuwa mwarobaini wa kupunguza gharama kubwa za kuagiza nje ya nchi, sambamba na kupunguza matumizi ya vibarua katika kuandaa mashamba, kupanda na kuvuna.

Kauli hiyo imetolewa leo, Jumatatu Aprili 27, 2026, na Mhandisi wa Karakana ya Kituo cha Uendelezaji wa Teknolojia, Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (Sido), Fredy Mapunda, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na hatua ya kuanza uzalishaji.

"Tulibaini kuwepo kwa changamoto ya mahitaji makubwa ya matumizi ya teknolojia na zana za kisasa katika uzalishaji, ndipo tukaja na wazo bunifu la kushirikiana na viongozi. Lengo ni kudhibiti upotevu wa mazao, kuongeza thamani na kukidhi mahitaji ya viwandani," amesema.

Amesema hatua hiyo imelenga kupunguza matumizi ya nguvu kazi kubwa ya wakulima katika uzalishaji na kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo, sambamba na uhakika wa upatikanaji wa malighafi viwandani.

Fundi Mkuu wa Kituo cha Uendelezaji wa Teknolojia katika  Shirika la Maendeleo ya Viwanda (Sido), Mkoa wa Mbeya, Japhet Mwakasonda akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Hawa Mathias

"Kwa wastani, kwa siku tunafikiwa na wakulima sita hadi 10, huku kwa mwaka wakiwa 2,190, lakini bado tunaendelea kupokea maombi ya zana za aina mbalimbali," amesema.


Manufaa

Ametaja miongoni mwa manufaa ya matumizi ya teknolojia za kisasa kuwa ni pamoja na mkulima kutumia muda mchache katika kufanya maandalizi ya shamba, kupanda, na kupunguza gharama za kutegemea vibarua.

Kwa upande wake, Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo (Sido) Mkoa wa Mbeya, Salma Galasi amesema kwa kutambua umuhimu wa kusaidia wakulima, wamebuni zana mbalimbali za teknolojia za kisasa katika uzalishaji zenye kuleta matokeo makubwa.

"Tumefanya ubunifu mbalimbali kuendana na mazingira. Lengo ni kuleta mapinduzi ya kweli katika sekta ya kilimo kama sehemu ya kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita katika kuchochea uchumi wa viwanda," amesema.

 Fundi Mkuu wa Kituo cha Uendelezaji wa Teknolojia Sido mkoani hapa, Mhandisi Japhet Mwakasonda, amesema lengo la kuja na teknolojia hiyo ni kuwaondoa wakulima katika matumizi ya jembe la mkono.

"Lengo ni kuona wakulima wanageukia teknolojia za kisasa katika uzalishaji ili kufikia malengo ya kuongeza thamani ya mazao na kukidhi mahitaji ya malighafi viwandani," amesema.


Kauli za wakulima

Daniel Mturo, mkulima kutoka Kijiji cha Iwindi Wilaya ya Mbeya, amesema ujio wa teknolojia hizo umempa hamasa ya kuongeza tija ya uzalishaji. Amebaini kuwa hapa nchini, kupitia Sido, zana hizo zinapatikana kwa kati ya Sh milioni 3, huku nje ya nchi zikiwa kati ya Sh milioni 10.