Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwakitinya: Kijana usidharau ujana wako, fikiria maendeleo

Vijana wametakiwa kutunza amani ya Taifa, wakikumbushwa wakiivunja hakuna kitu kitakachofanyika ikiwamo shughuli za kujiingizia kipato, masomo na masuala yote ya kijamii.

Huku wazazi wakipewa jukumu la kusema na vijana wao badala ya kuwaacha wafunzwe na ulimwengu kwa kujaribu kuchezea amani ya Taifa kwa kuandama.

Rai hiyo imetolewa jana Oktoba 27, 2025, na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara, Mussa Mwakitinya, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ikiwa ni katika mwendelezo wa kunadi ilani ya chama hicho na kumuombea kura mgombea urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan.

Mwakitinya alisema vijana wasihadaike na hamasa inayofanywa mitandaoni ya kutomasa amani ya nchi na watu waliopo nje ya nchi au kwingineko ambao hawataathirika kwa vyovyote na kitakachotokea.

“Vijana wenzangu wa Taifa la Tanzania yeyote asidharau ujana wake wapo watu wanahamasisha vijana waingie barabarani wafanye maandamano wapate maafa ilihali wapo nje ya nchi, kuna vijana wanaweza wakatumika kuiharibu au kutomasa  amani ya Taifa la Tanzania.”

Alisema kwa pamoja watakwenda kuilinda amani ya Taifa.

“Tuendelee kuitunza amani ya Taifa letu tukijua hatua Taifa lingine la kwenda isipokuwa mama la  Tanzania. Hapa  ndipo tulipozaliwa, tuliposoma au tunaposoma na tunakofanya shughuli zetu za kiuchumi. Amani ya Taifa ikiharibika hatutaweza kukaa vizuri kufanya shughuli za maendeleo,”amesema Mwakitinya.

Akifafanua zaidi Mwakitinya alitumia msemo wa wahenga usemao: ‘Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu’, akiwasihi vijana kutojiandaa kufunzwa na ulimwengu badala yake wasikilize wanachoambiwa.

“Wazazi mmetuzaa, mmetulea  wenyewe tunaotukana mitandaoni mnatujua na tunaohamasisha vurugu mnatujua kaeni na sisi mtuonye kabla hatujafunzwa na ulimwengu,”alitoa rai Mwakitinya.