Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Doyo aibua mambo matano Geita, akiomba ridhaa

Muktasari:

Baada ya Geita, msafara wa kampeni wa Doyo unaelekea mkoani Kagera, Wilaya ya Ngara, kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo na kuomba ridhaa ya kuichagua NLD kwenye uchaguzi mkuu.

Dar es Salaam. Mgombea urais wa NLD, Doyo Hassan Doyo ameibua mambo matano aliyoyataja kuwa ni kero katika Mkoa wa Geita, ambayo ameahidi kuyashughulia endapo Watanzania watampatia ridhaa kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 29, mwaka huu.

Katika muendelezo wa kampeni zake mikoa ya  Kanda ya Ziwa leo Septemba 30, 2025  zilizofanyika katika Jimbo la Sengerema, eneo la Stendi ya Zamani na Kata ya Buseresere, Mkoa wa Geita, Doyo amesema kero kubwa katika maeneo hayo ni ubovu wa barabara na gharama kubwa za usafiri.

Ameitaja kero nyingine ni ukosefu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya, upungufu wa maji safi na salama na changamoto ya wakulima kushindwa kupata masoko yenye tija kwa mazao yao.

Amesema endapo wananchi wataridhia mikakati iliyomo kwenye Ilani ya chama chao na wakamchagua kuongoza nchi, kipaumbele chake ni kwenda kuzikomesha katika mwaka wake wa kwanza madarakani.

Doyo amewaomba wananchi wa Kanda ya Ziwa kutafakari kwa kina juu ya sababu zinazowafanya kuendelea kukosa maendeleo, akigusia namna wakulima wanavyolazimika kuuza mazao yao katika masoko yanayowanyonya.

"Mkinipa ridhaa nitahakikisha wakulima wanapata fursa ya kuuza mazao yao katika masoko yenye tija na faida, hivi sasa wengi wanalazimishwa kuuza katika masoko yanayowanyonya na kuendeleza umaskini.

“Wananchi, mkiniamini na kunipa kura Oktoba 29, nitasimamia na kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri na zenye motisha kwenye mazao yenu yote,” amesema Doyo.

Amesema haiwezekani wananchi watumie gharama kubwa katika kilimo, halafu Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inawapangia bei.

Mgombea urais huyo amesema hizo ni mbinu za chama hicho kutaka kuendeleza umaskini kwa wananchi kusudi waendelee kutawaliwa.

Katika kampeni hizo, Doyo aligusia pia changamoto za miundombinu na huduma za kijamii wilayani Sengerema, akibainisha kuwa licha ya taifa kuwa na rasilimali nyingi kama dhahabu, almasi na Tanzanite, bado wananchi wanaendelea kuishi maisha ya umaskini.

“Nchi hii ina madini ya kila aina, lakini bado wananchi wake hawana maji safi, huduma bora za afya na miundombinu ya barabara. Hili ni jambo la aibu kubwa,” amesema Doyo.

Mgombea huyo amegusia pia sekta ya usafirishaji, akibainisha madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji wanalalamikia gharama kubwa za uendeshaji kutokana na ubovu wa barabara.

"Hali hii inasababisha biashara zao kushindwa kuleta faida huku wakidaiwa kodi kubwa bila kuhakikisha uwekezaji kwenye barabara unafanyika ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato.

"Changamoto hizi zimeshindwa kutatuliwa kwa miongo kadhaa, na sasa wanarudi tena kwa wananchi kuomba kura kwa hoja zilezile ambazo hawajawahi kuzitekeleza, Watanzania ichagueni NLD kwa maendeleo,” amesema.

Awali, akimnadi mgombea urais huyo, Kampeni meneja wa NLD, Pogora Ibrahim Pogora amesema Watanzania wanapaswa kumchagua mgombea huyo kwa kuwa amejipambanua kuwa kiongozi atakayetetea maslahi yao.

"Ni wakati wa wananchi kumchagua Doyo, kiongozi atakayekwenda kutatua changamoto zenu ambazo kabla ya kuomba ridhaa yenu amezifanyia utafiti changamoto hizo," amesema Pogora.

Amesema Ilani ya NLD imezingatia mambo matatu ambayo ni uzalendo, haki na maendeleo, ambavyo mzalendo wa kweli Doyo atavisimamia na kuvitekeleza ipasavyo Watanzania wakimpa ridhaa kwenye Uchaguzi