Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TCC Plc inavyojipambanua katika uimarishaji usalama na afya kazini

Uongozi na wafanyakazi wa TCC Plc wakisherehekea moja ya kampeni za usalama kwenye eneo la kiwanda.

Kwa kuwa uchumi wa nchi haujengwi na watu wasio salama kimwili na kiakili, Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC Plc) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kusimamia utekelezaji wa kanuni za usalama na afya mahala pa kazi kwa asilimia mia moja na zaidi.

Ukiwa TCC Plc, usalama unaanza kwanza kabla ya mambo mengine. Mwandishi wetu amefanya mazungumzo na Meneja Usalama, Afya na Mazingira TCC Plc, Protas Kangalawe kuhusiana na uzingatiaji usalama na afya kazini na hii ni sehemu ya majibu yake:

Swali: Hatua gani mmeshazichukua kuonyesha utayari kukabiliana na vihatarishi vya kiusalama ikiwamo mabadiliko ya tabianchi?

Katika hatua muhimu ya kuboresha usalama barabarani, mwanzoni mwa mwaka huu, TCC Plc ilizindua rasmi programu ya “Brightmile” kwa watumiaji wa magari ambayo inalenga kuongeza ufahamu wa usalama na kutoa jukwaa la maswali ya wafanyakazi.

Ukaguzi wa usalama pia ulifanywa, jitihada hii ilisisitiza msimamo wetu kuhusu usalama, bila kujali changamoto za hali ya hewa, na kuhakikisha mahali pa kazi ni salama na penye taarifa kwa wote.

Uzinduzi huu wa kimkakati unasisitiza dhamira ya kampuni ya kuboresha usalama barabarani na kujenga tabia njema za uendeshaji kulingana na ahadi yake ya usalama barabarani.

TCC Plc inatoa mafunzo ya usalama wa moto na dharura kwa baadhi ya wafanyakazi wake, kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji. Programu hii imeimarisha kwa kiasi kikubwa uwezo wetu wa kudhibiti dharura za moto.

Mpango huu unaashiria hatua nyingine muhimu katika juhudi zetu zinazoendelea kuhakikisha usalama na ustawi wa timu yetu, na hivyo kuifanya TCC Plc kuwa kiongozi katika usalama mahali pa kazi.

Swali: Mnalindaje mnyororo wa uzalishaji wenu kuanzia kwa wafanyakazi na wakulima wa tumbaku kuhakikisha hawaathiriwi kwa kiasi kikubwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi?

TCC Plc ni kampuni inayofanya kazi kwa kufuata kanuni za ISO 45001 na 14001, kupitia viwango elekezi vya mifumo ya ISO, imetuwezesha kufanya mipango na mikakati yenye kuzingatia mnyororo mzima wa shughuli zetu za uzalishaji.

Hivyo kwa kushirikiana na kampuni dada ya JTI Leaf Services, Tabora, tumeweza kutambua vihatarishi vya kiusalama na kimazingira vinavyoweza kutokea kwenye operesheni zetu mashambani, lakini pia usafirishaji wa malighafi, uzalishaji kiwandani pamoja na usambazaji wa bidhaa hadi kumfikia mteja wetu.

Swali: Mnatumia njia gani kupima hatari na kufanya tathmini za athari zinazoletwa na janga katika shughuli zenu?

Kupitia nyenzo kama tathmini ya vihatarishi (Risk Assessment) pamoja na nyenzo na programu zingine, TCC Plc imefanikiwa kufanya shughuli zake huku ufanisi kwenye uzalishaji pamoja na kuhakikisha usalama kwenye kila hatua ya uzalishaji.

Hivi karibuni, TCC Plc imeanzisha mfumo wa kuondoa matukio ya ajali (Incident Elimination) kupitia mfumo huu, tathmini za hatari hufanyika kila mwanzo wa shifti, pamoja na mfumo wa kuchunguza tabia za ufanyaji kazi.

Swali: Mmewaandaa kwa kiasi gani wafanyakazi wenu kukabiliana na majanga mengine ya asili? Na utayari wao upo kwa kiasi gani kwa tathmini fupi kwa mwaka huu 2024?

Kupitia utaratibu ulioandaliwa wa matayarisho ya dharura/ majanga na jinsi ya kukabiliana nayo (Crisis Management and Emergency Preparedness and Response Procedures), kampuni inafanya mafunzo ya mara na mara kwa wafanyakazi kuhakikisha wako tayari kwa majanga yote ya asilia, na jinsi watakavyokabiliana nayo yakitokea.

Swali: Mnashirikiana na taasisi gani kukabili na kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi katika shughuli zenu?

Tunafanya tathmini ya mazingira kila robo ya mwaka, kujihakikishia kwamba mazingira yetu ya kazi yako katika viwango elekezi kisheria, kwa kushirikiana na wasimamizi wa sheria hizi ambao ni OSHA pamoja na NEMC.

Swali: Nini mnajivunia katika mifumo yenu ya usalama na afya mahala pa kazi?

Wafanyakazi wenye kiu ya kutaka kujifunza zaidi na wenye kutoa ushirikiano kwa kutoa mirejesho na maoni ya kuboresha zaidi mifumo yetu. Kuongezeka kwa ushiriki wa wafanyakazi (Engaged workforce) hivyo kuonyesha uwezo wa juu na uelewa kwenye masuala ya usalama na afya.

Swali: Fursa gani mnaziona katika kuendelea kuimarisha uwezo wenu wa kushughulikia usalama na afya kwa siku zijazo?

Usalama ni jukumu la kila mmoja, hivyo tunajivunia kupitia kampeni yetu endelevu ya “Usalama Unaanza Na Mimi” yenye kuhamasisha umiliki kuanzia ngazi ya mfanyakazi wa chini kabisa hadi kwenda kwenye timu ya uongozi.

Lakini pia kuendelea kuhamasisha mazungumzo ya kiusalama ni kipaumbele chetu, kuhakikisha usalama unazungumzwa kila wakati kwenye vikao vyote ni lazima kuanza na ajenda ya usalama, lakini katika operesheni suala lote la usalama lisifumbiwe macho.

Swali: Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahala Pa Kazi duniani mwaka huu yalibeba kauli mbiu inayohimiza utafutaji suluhu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi mahala pa kazi. Hili mnalitekelezaje kwa vitendo kama moja ya wadau?

Tulifanya tathmini ya mazingira yetu ya kazi, kujihakikishia kwamba mazingira yetu ya kazi yako katika viwango elekezi kisheria.

Lakini kikubwa ambacho kimefanyika mwaka huu ni maboresho ya mfumo wa hewa mfunguko (Air circulation system) hivyo kuendelea kuboresha hali ya hewa kwenye maeneo ya kazi.

Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa nchi nyingi zinazotegemea sekta za uzalishaji zinazotumia rasilimali watu wengi ikiwamo viwanda.