Kikosi cha Simba kimewasili jijini Dar kikitokea Zanzibar baada ya kutolewa kwenye michuano ya Mapinduzi.
Kocha mkuu mpya Robertinho Oliveira wakati anatambulishwa uongozi wa Simba ulisema endapo wangetolewa basi watatafuta kambi Tanzania au nje ya nchi kwa ajili ya kujiandaa na michuano mingine ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu NBC na Kombe la Azam Shirikisho.